Wednesday 3 October 2012

Vigogo CCM ‘wahamia’ Marekani

• Ni JK, Mkapa, Kinana, Membe na Nape
 
VIGOGO watano wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wako nchini Marekani, Tanzania Daima Jumatano limebaini.
Uwepo wa vigogo hao Marekani kwa wakati mmoja, umeibua gumzo nchini hususan kwa mitandao ya makada wa chama hicho wanaotajwa kutaka kuwania urais mwaka 2015.
Vigogo hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, na mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC), Abdulhaman Kinana, ambaye amepata kuwa kampeni meneja wa marais hao wawili.
Mwingine ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa makada watakaowania urais mwaka 2015.
Wakati vigogo hao wako nchini Marekani, kigogo mwingine wa CCM, Nape Nnauye, ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, anatarajia kwenda nchini Marekani kesho.
Ingawa vigogo hao wako Marekani kwa shughuli na sababu tofauti, mahasimu wa Waziri Membe kisiasa wamehusisha ziara hiyo ya wazito hao na harakati za urais 2015.
Rais Kikwete yuko nchini Marekani kwa ziara ya kikazi. Rais na ujumbe wake uliondoka nchini juzi na atakuwa hapo kwa siku mbili kabla ya kuelekea nchini Canada kwa ziara nyingine rasmi ya kiserikali.
Habari zinasema kuwa Mkapa na Kinana waliondoka nchini wakati vikao vya mchujo vya CCM vikiendelea mjini Dodoma na wako nchini humo kwa ajili ya shughuli za taasisi ya Mkapa Foundation na Nape anatarajia kwenda kwa shughuli zake binafsi.
Hadi sasa hakuna kada yeyote wa CCM aliyetangaza kuwania urais, lakini mbali ya Membe, duru za kisiasa zinawataja makada wengine wanaotaka urais kuwa ni pamoja na mawaziri wakuu wastaafu, Frederick Sumaye na Edward Lowassa.
Hata hivyo, kasi ya Sumaye kuwania nafasi hiyo imepunguzwa na matokeo ya uchaguzi wa NEC, wilayani Hanang’ ambapo aliangushwa na Dk. Mary Nagu.
Wengine ni Samuel Sitta, Dk. Abdallah Kigoda, Dk. Emmanuel Nchimbi, Dk. Asha Rose Migiro na wengine.
KWA HABARI KAMILI TEMBELEA:
 

No comments:

Post a Comment

Chadema UK Ndani ya Milton Keynes

DAR NI SISI - VIDEO MAISHA YA WANADAR HATA BAADA YA MIAKA50 YA UHURU