Sunday, 30 September 2012

Mbowe afichua siri mgogoro wa RC, madiwani Moshi

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema mvutano uliopo kati ya madiwani wa Manispaa ya Moshi na Mkuu wa Mkoa (RC) wa Kilimanjaro ni mpango wa serikali kutotaka kuziachia halmashauri zinazoongozwa na chama hicho kufanya kazi zake mipango iliuyojiwekea.
Mbowe alisema kuruhusu wakuu wa serikali kupindisha maamuzi ambayo yamefanywa na vyombo hivyo vilivyopo kisheria, ni kujenga utawala wa kiimla katika taifa kwa kujiongoza kwa matamko au mapenzi ya viongozi badala ya kanuni za halmashauri.

Alisema kisheria Baraza la Madiwani linajiendesha kwa kanuni na sheria, kwa mamlaka walizopewa madiwani na wananchi, hivyo wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kuviheshimu vikao hivyo na siyo kuruhusu kutumika na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuvuruga upinzani hata kwa kuvunja kanuni.


Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, alisema mvutano uliopo sasa katika Baraza la Madiwani linaloongozwa na CHADEMA na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, ni ushuhuda mwingine wa matumizi yaliyovuka mipaka ya kimadaraka ambayo yamekuwa yakifanywa na wakuu wa wilaya na mikoa kuvuruga halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA.


“Ndiyo maana sisi kama CHADEMA tunasema kuwa suluhu ya matatizo haya yote ni katiba mpya, kwani cheo cha mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ni vyeo vya kufutilia mbali, kwanza mtu anayeteuliwa na rais hana maslahi yoyote kwa mwananchi badala yake ni kuwaingilia viongozi waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kuvuruga amani na kushindwa kufanya kazi za maendeleo,” alisema Mbowe.


Alisema tatizo kubwa lipo kwa wakuu wa serikali kuruhusu kutumika na CCM ili kuleta chokochoko kwa mabaraza yanayoongozwa na CHADEMA, huku akitolea mfano mabaraza ya Hai, Arusha, Mwanza na Moshi ambapo kanuni zimekuwa zikivunjwa makusudi ili kusababisha madiwani waliochaguliwa na wananchi kushindwa kufanya kazi zao.


“Ukweli ni kwamba vikao vya halmashauri vipo kisheria na vinaweza kufanya maamuzi yake, lakini wakati mwingine vikao hivi vinaweza kuwa na madhaifu, hivyo ni vema mkuu wa mkoa na meya wakaitana mezani na kushauriana, kwani kuvutana kunakuwa hakuna mantiki yoyote.


“Kama ni matumizi mabaya ya fedha CCM imekwishafanya ubadhirifu mkubwa sana wa fedha ambao ulifanywa na viongozi tena wa chama hicho, najua huu ni mpango unaofanywa na CCM, lakini mimi Mbowe nasema CHADEMA itaendelea kujenga demokrasia ya haki kwa kuendelea kutamalaki kwa kupewa mamlaka na wananchi wenyewe, na siyo vinginevyo,” alisema Mbowe.


Mvutano uliopo kwenye Manispaa ya Moshi ni ule wa Mkuu wa Mkoa kuzuia safari ya madiwani, na watendaji kwenda Kigali Rwanda, safari ambayo ilikuwa igharimu sh milioni 123. Pia mkuu huyo alipingana na gharama hizo kwa kusema ni ndogo kwani itagharimu zaidi ya milioni 200.


Hata hivyo, Mbowe alisema kuwa kama madiwani wamekaa na kuona kuna umuhimu wa wao kufanya safari hiyo, ni vema mkuu wa mkoa angeheshimu maamuzi yao, kwani kama utaratibu huo ukiendelea madiwani waliochaguliwa na wananchi watashindwa kufanya maamuzi yao kwa kuongozwa na matamko kutoka kwa viongozi wa serikali.

uzi wa leo kutoka Jamii Forums

Wasira awakana watoto wake waliojiunga na chadema

Kutoka Gazeti la Mwananchi

Kashfa nyingine yaibuka Tanesco

KASHFA mpya imeibuka ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), baada ya kubainika kuwa vikombe vya kufungia nyaya za umeme vyenye thamani ya mamilioni ya fedha vimetelekezwa kutokana na baadhi ya vigogo wa shirika hilo kushindwa kunufaika na mradi huo.

Habari kutoka ndani ya shirika hilo zinaeleza kuwa vigogo hao wanadaiwa kuvikataa vikombe hivyo kwa maelezo kuwa ni vibovu, baada ya mzabuni kushindwa kuwaona vigogo hao.

Wakati vigogo hao wakivikataa vikombe hivyo kwa madai kuwa ni vibovu, taarifa zinaeleza kuwa wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamethibitisha kuwa vikombe hivyo ni vizuri na havina matatizo yoyote.

Hatua ya Tanesco kupeleka vikombe hivyo kuthibitishwa na wataalamu wa Chuo Kikuu, Kitengo cha Uhandisi ilitokana na mvutano uliokuwapo baada ya vigogo walioshindwa kunufaika na mradi huo kutoa maelezo kuwa vikombe hivyo havina viwango bora.

Hata hivyo, uchunguzi unaonyesha kuwa licha ya vigogo hao kuvikataa vikombe hivyo zaidi ya 40,000 vyenye thamani ya Sh900 milioni kwa madai kuwa vibovu, tayari shirika hilo limekuwa likivitumia katika nguzo zake zenye umeme mkubwa kwa miaka mingi.

Familia ya Waziri Wasira yahamia Chadema

Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbroad Slaa akiwakabidhi kadi za uanachama wa CHADEMA watoto wa Wasira
 
Yadai inahitaji mabadiliko ya kweli
Yasisitiza udugu utabaki pale pale
WATOTO wa kaka yake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Uhusiano na Uratibu, Steven Wassira wametangaza kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Kwa mujibu wa watoto hao, uamuzi wao wa kujiunga CHADEMA unatokana na kuona nuru ya mabadiliko kupitia chama hicho.

Vijana hao, Esther Wassira na Lilian Wassira ambao ni watoto wa George Wassira, walijiunga na chama hicho jana.

Walipokewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Dar es Salaam.

Vijana hao ambao ni wanasheria, wamaliki Kampuni ya Uwakili ya Armicus Atorneys.

“Tuna haki ya kuchagua chama cha kujiunga nacho,Wassira ni baba yetu mdogo na atabaki kuwa hivyo lakini sisi tuna hiari ya kufanya kile tunachokiamini,”alisema Esther.

Esther ambaye ni mdogo wa Lilian, alisema hivi sasa Tanzania inahitaji mabadiliko ya dhati kwa kuunga mkono Vuguvugu la Mabadiliko (M4C kuondoa kero zinazokwamisha maendeleo nchini kwa zaidi ya miaka 50 sasa.

“Kwa mara ya kwanza nimeamua kujiunga na M4C, naiona CHADEMA ni chachu ya mabadiliko. Ni wakati mpya kukiweka chama hiki kwenye uso mwingine wa siasa.

“...huu ni mfumo wa vyama vingi, hatuwezi kuendelea na CCM ambayo siku zote inacheza ‘muziki’ na kufuata nyayo za Chadema. Bila shaka ni chama chenye sera nzuri.

“Sisi kama vijana tunaona bado tunayo nafasi ya kufanya kitu kupitia Chadema, lazima nifanye kitu kwa ajili ya nchi yangu naamini wanaweza kutufikisha pale tunapotaka,” alisema Esther.

Naye Lilian alitoa wito kwa Watanzania kuamini mabadiliko ya maendeleo yanawezekana kupitia chama hicho.

“Naamini hatujapotea, tuko sahihi na tumeingia chama sahihi, tunaona wanavyopambana, tumeamua kuwa sehemu ya mabadiliko… sifuati ukongwe wa chama bali sera zenye matumaini ya dhati kwa ajili ya kizazi chetu Watanzania.

“Tukiunganisha nguvu Tanzania mpya inakuja, bila madadiliko hakuna ushindani. Tunataka maendeleo, tumechoshwa na sera za CCM, naamini kwa msaada wa Mungu inawezekana,” alisema Lilian.

Akizungumza baada ya kuwapokea, Dk. Slaa alisema hatua yao hiyo ni kielelezo tosha kwamba yale yanayozungumzwa na CCM kupitia kwa Wassira kuwa Chadema ni chama cha vurugu na fujo ni propaganda zilizopitwa na wakati.

“Siamini watu wenye akili timamu kama vijana hawa wanaweza kujiunga na chama ambacho ni cha fujo na vurugu kama ambavyo imekuwa ikisema kwa nguvu kubwa na kupitia kwa Wassira,”alisema Dk.Slaa.

Kuhusu chama hicho kudaiwa kuwafanyia vurugu wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF) mkoani Arusha, Dk.Slaa alisema si haki kukihusisha chama hicho na vurugu hizo kwa sababu hakina hatimiliki na Arusha.

Alisema si kila mfanyabiashara ndogo ndogo (machinga) ni mwana Chadema.

“Kumezuka na upotoshaji kujenga dhana kwamba kila machinga wa Arusha ni mfuasi wa CHADEMA. Sisi hatuna hatimiliki Arusha, kila chama kinayo haki ya kufika kila kona ya nchi hii kufanya siasa bila kuingiliwa, lakini wasituhusishe na vurugu za CUF,” alisema Dk.Slaa

Mkutano wa Zitto Kabwe Karatu Mjini

Mdee Afungua Shina La CHADEMA Boko
Mdee `amshukia` Mchungaji Lwakatare

Serikali imetakiwa kumdhibiti na kumuondoa, kisha kuibomoa nyumba ya Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mchungaji Getrude Lwakatare.
Rai hiyo imetolewa na Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee.
Taarifa kwa vyombo vya habari jana ilieleza kuwa, wakati raia wengine wakibomolewa nyumba ambazo kama ilivyo ya Mchungaji Lwakatare, zilijengwa kinyume cha sheria, Mbunge huyo amehamia na kuishi kwenye nyumba yake.
Julai mwaka huu, nyumba za wananchi waliojenga katika maeneo tengefu ya ufukwe wa Jangwani, mto Ndumbwi na mto Mbezi, zilibomolewa katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (Nemc).
Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta nane. Lakini nyumba ya Mchungaji Lwakatare haikuguswa.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk Terezya Huvisa, aliwahi kuwaambia waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, nyumba hiyo haikubomolewa kutokana na pingamizi la mahakama.
Nyumba inayotajwa kuwa mali ya Mchungaji Lwakatare, imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za bahari ya Hindi.
Viwanja hivyo vinadaiwa kupatikana kwa ushirikiano wa Mchungaji Lwakatare na Frank Mushi.
Mdee alisema wakati kigogo huyo (Lwakatare) amehamia kwenye nyumba yake kwa matangazo na mbwembwe, mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa, lakini zaidi kuwepo raia waliobomolewa kwa mujibu wa sheria hizo.
Mdee alinukuu Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004, fungu 57(1), inasema hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60.
Mita hizi ni ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri ulinzi na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa bahari, kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili wa ziwa.
Sheria nyingine ni ya ardhi, namba 4 ya mwaka 1999, sura 113, fungu la 7 (1) (d), ikieleza kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka kingo ya mto na bahari, linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa.
Na pale inapotokea kuwa masharti ya sheria moja yanapingana na masharti ya Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa mazingira, sheria hiyo inatumika, kwa mujibu wa fungu 232 la sheria ya mazingira sura 191 ya mwaka 2004.
”Kutokana na hali hii, serikali inatakiwa kujinasua katika mwendelezo wa tafsiri wanayoipata wananchi kuwa imetekwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache wenye uwezo,” alisema.
Aliongeza,” maana wanaona kuwa huu ni mwendelezo wa serikali kuwa na kigugumizi pale sheria zinapovunjwa na vigogo serikalini, au watu wenye fedha wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala kufanya ufisadi.”
Alisema hali ilivyo sahihi inadhihirika kuwepo kundi la wanaojiona wapo juu ya sheria, huku wanyonge wakishughulikiwa.
”Ni wakati kwa mawaziri wanaohusika na masuala ya ardhi na mazingira kuwaeleza Watanzania kulikoni wananchi wa hali ya chini kuvunjiwa nyumba wakati Mchungaji Lwakatare, ambaye uharibifu wake ni wa hatari kuliko waliovunjiwa akitamba mtaani, ” alidai.
Mdee alitafsiri kitendo hicho kama ni Mchungaji Lwakatare kutamba kuwa yuko juu ya sheria na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kumzuia kufanya alichofanya.
”Ni aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa aina hii! Viongozi ambao wako tayari kutumia fedha, hila, mamlaka na dhamana za uongozi walizopewa, kuhalalisha haramu, ni janga kwa mstakabali wa taifa letu,” alisema.
Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, hawakupatikana kuelezea juu ya tamko la Mdee.
Mawaziri hao walikaririwa kwa nyakati tofauti wakisema nyumba zote zilizojengwa kando kando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa

TAMKO LA CHAMA KUKANUSHA SHUTUMA ZA CHAMA CHA CUF KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA.

TAMKO LA CHAMA KUKANUSHA SHUTUMA ZA CHAMA CHA CUF KUFANYIWA VURUGU NA CHADEMA.
Ndugu wananchi na wanahabari,

Siku ya terehe 27 Alhamisi Septemba 2012 chama cha wananchi CUF walitoa taarifa ya malalamiko kwa vyombo vya habari na mitandao kuwa wanachama wa CHADEMA wamewafanyia vurugu kwa kuwapiga mawe na kuwa jambo hilo limehamasishwa na viongozi wa chama katika mkoa wa Arusha pamoja na Mhe Godbless Lema.
Wote tunafahamu kuwa siku hiyo hiyo katika viwanja vya soko la Kilombero wafanyabiashara ndogo ndogo walikuwa wamevamia na walikuwa wakijigawia maeneo, baada ya eneo la awali walilopewa la viwanja vya NMC kushindwa kuwachukua wafanyabiashara wote na halmashauri kushindwa kutoa majibu kwa wafanyabiashara hawa ambao waliwaambia wote waende NMC.
Kwanza tunapenda kutoa pole kwa viongozi wa CUF kwa jambo hili lililowapata. Wao kama watu na Watanzania wenzetu tunawapa pole sana.
Pili, CHADEMA inakanusha kuhusika na jambo hili. Hii si tabia ya CHADEMA na kamwe haiwezi kuwa tabia ya CHADEMA kufanya siasa chafu za namna hiyo. CHADEMA tunajali sana amani na upendo, na hii ndiyo tabia na makuzi yetu Watanzania.
Katika mazingira haya, CHADEMA tunachukua fursa hii kuvikaribisha vyama vyote mathalani CUF, Arusha ni yetu sote na tutumie demokrasia vizuri kufanya kazi nzuri ya siasa kwa ajili ya kusababisha na kuleta matumaini kwa Watanzania hawa ambao serikali ya chama cha mapinduzi imeshindwa kuwaletea.
CHADEMA hatuna shida na ushindani wa kisiasa katika mazingira ya kidemokrasia kwa maana ndio wakati pia wa wananchi kupima na kujua nani mkweli na ama nani anafanya kwa dhati ya kweli. Hivyo tunawakaribisha CUF karibuni Arusha na wala wasitafute kisingizio cha kuegemea ili CUF ianze kutajwa tajwa kwa kutumia mgongo wetu.
Sambamba na hili, CHADEMA mkoa wa Arusha tumesikitishwa sana na tamko la CUF lilitolewa na Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na haki za BInadamu Mhe Abdul Kambaya, tamko lenye matisho na lugha isiyofaa. Moja na maneno ya tamko hilo wamesema, nukuu “Uwezo wa kuwafanya tutakavyo tunao na kwa sababu wameanza tunaweza kumaliza”. Wakazi wa Arusha na Watanzania wapime na waone, haya si maneno yanayoweza kutoka kwenye kichwa cha mtu anayefikiri vizuri, mtu anayeipenda nchi yake na kuheshimu utawala wa sheria. Zaidi ya hapo tamko hilo limesema pia, “Ile ngangari kwa polisi tunaweza kuwahamishia wao wakose pa kukaa”.
Katika yote haya, niwaombe wakazi wa Arusha, Wanachadema na hata wanachama wa vyama vingine tuwapende na tuwakaribishe CUF Arusha na sote tufanye kazi ya siasa kwa nguvu za hoja. CUF wanaweza kufanya hicho wanachotaka kufanya lakini CHADEMA kamwe hatupo tayari kwa vurugu ya aina yoyote, aidha tunawakaribisha kwa moyo mmoja na kama wapo tayari basi tufanye siasa zenye tija na manufaa kwa wakazi wa Arusha.
Aidha nitoe onyo kali sana kwa mamluki ambao wamekuwa wakijifanya kondoo kumbe ndani ni mbwa mwitu. Mara kadhaa watu hawa wamekuwa wakisababisha fujo ili kukifanya CHADEMA kionekane kuwa ni chama cha vurugu. MAMLUKI ni sumu, tukimgundua na kumthibitisha mtu wa aina hiyo katikati yetu tutamtangaza mbele ya jamii kuwa yeye ni sumu na kuomba wananchi wamtenge maana anapingana kwa kuleta hila na unafiki kwenye kazi ya kuwakomboa Watanzania. Niwatangazie mamluki hamtatuweza na tutawagundua tu.
Mwisho, tunapoelekea kwenye marudio ya uchaguzi mdogo kwenye kata za Daraja II kwa Arusha mjini na Bangata kwa wilaya ya Arumeru Magharibi, nirudie kusema maneno ya Mhe Lema kuwa iwapo viongozi na watumishi wa umma watajihusisha na kushiriki kwa kufanya kampeni za kisiasa wakiwa wanatumia magari na vifaa vingine vya serikali watu hawa tutawakamata na tutawapeleka huko wanakostahili kupelekwa wezi na vibaka wengine. Hii ni tahadhari tunamaanisha kweli na wananchi wote wawe makini “wakamate mwizi” lengo likiwa ni kuweka adabu kwa watumishi na viongozi umma wanaovunja sheria ya utumishi wao kwa umma na matumizi ya rasilimali kwa namna isivyotakiwa kisheria. CHADEMA tutashiriki chaguzi hizi na tunawaomba wakazi wote wa maeneo haya tushiriki kwa utulivu na amani.
WANACHADEMA wote tuendelee kuwa majasiri, tusiwe waoga na tusimamie kweli na haki.
“Hakuna kulala Mpaka Kieleweke”
Amani Sam Golugwa
KATIBU WA CHADEMA MKOA WA ARUSHA: golugwa@gmail.com

John Heche afichua mbinu chafu zinazoelekezwa kwa Chadema


 
Mpango wa kusitisha M4C, baada ya ccm kugundua kwamba mbinu zote za kusitisha M4C kwa kutumia polisi na dola zimegundulika baada ya kujaribu kutumia vifo vya Morogoro na Iringa kushindikana sasa wameamua kuwatumia CUF, mpango unaonyesha kwamba CUF watakwenda kwenye maeneo ambayo chadema ina nguvu kubwa sana kama Arusha, Mbeya, Mwanza, Manyara, Kiliman jaro,morogoro, Shinyanga,Mara na maeneo mengineyo
 
 

Mbali na hilo watafanya mikutano ambayo itakua na lugha za matusi na kejeli na kuikashfu Chadema na viongozi wake ili wapenzi na wanachama wa chadema wawafanyie fujo hao wanaotukana au watumie watu watakaovalishwa nguo za chadema kuanzisha fujo kwenye mikutano ya CUF ili ionekane kwamba CUF wanafanyiwa fujo baada ya kuoneka hivyo Cuf watawataka wanachama wao pia kuifanyia chadema fujo na hivyo serikali itaingilia kati kufuta operesheni M4C na kile kilichoanzishwa na CUF kwa jina la V4C na malengo ya ccm kutuzuia kwenda vijijini kuwaamshaWatanzania yatatimia kwa kutumia justification kwamba mikutano hiyo inafujo kwahiyo imefutwa au kusitishwa na hapo CUF watakubali kwa haraka maana ni mpango wa pamoja, nachukua fursa hii kuwaomba vijana wa Chadema popote walipo wasifanye fujo au hata kutukana mtu hata wakifanyiwa fujo wasijibu maana tutawapa fursa wabaya wetu kutumaliza, tunaikaribisha sana CUF popote ili wajipime na kuona je ni washindani wetu kweli? sisi hatushindani na CUF wala chama kingine chochote cha upinzani bali adui yetu ni ccm, ninawaomba viongozi wa vyama vya upinzani hasa Cuf kuacha kutumiwa na dola kufifisha harakati za watanzania kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi hii kwa kutumia chama chao cha demokrasia na maendeleo chadema.

MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA, HAKUNA KULALA MPAKA KILEWEKE

Tuesday, 25 September 2012

CHADEMA: Kama safari ya kifisadi RC atushitaki

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Manispaa ya Moshi kimemtaka Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, kutumia vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwashitaki madiwani kwa kile anachodai ufisadi uliotaka kufanywa na madiwani hao katika safari yao ya mafunzo Kigali nchini Rwanda.
CHADEMA kupitia makada wake maarufu, James ole Millya na Jafary Michael walitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa mikutano ya hadhara iliyoanza hivi karibuni katika maeneo mbalimbali ya mji wa Moshi kutoa ufafanuzi kwa wananchi wa hatua ya mkuu huyo wa mkoa kuzuia safari hiyo huku wakiita ni ya kisiasa zaidi.

Mapema mwezi huu, Gama aliwaambia waandishi wa habari mbele ya kamati ya ulinzi ya mkoa kuwa amesitisha safari hiyo ambayo ingegharimu sh milioni 123.2.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penford vilivyoko katikati ya mji wa Moshi, Meya wa manispaa hiyo, Jafary Ally, alisema fisadi yeyote anapothibitika anachukuliwa hatua za kisheria.

“Ndugu zangu wananchi wa Moshi, kama kweli Gama anaona kile madiwani wa CHADEMA walichotaka kukifanya ni ufisadi….. leo hii hakuna hata mmoja wetu ambaye angekuwa katika eneo hili la mkutano, wote tungekuwa gerezani.

Alisema mkuu huyo wa mkoa sasa ameacha majukumu yake ya kiserikali na kuanza kutumika kisiasa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuwagombanisha madiwani hao ambao wengi wao wanatoka CHADEMA.

Meya Michael alisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo madiwani zitatumika kama zilivyopangwa na kama mkuu huyo wa mkoa akiendelea kutumika kisiasa na kuacha shughuli za utendaji wa kuwatumikia wananchi, watatangaza mgogoro naye wa kutoshirikiana kwenye shughuli zozote.

Tanzania Daima

CHADEMA kuzindua matawi kila kata

 
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuzindua matawi katika kila kata nchini, ili kujihakikishia ushindi wa asilimia kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka 2014 nchi nzima.

Kauli hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, katika ziara ya ufunguzi wa matawi na msingi 10 ya chama hicho kata ya Kimara.

Akizindua tawi la Kilungule ‘B’, Mnyika aliwaambia viongozi wa matawi hayo kuziona ofisi hizo kama mbadala wa ofisi za Serikali za Mtaa zinazoongozwa na CCM kwa kuwasaidia wananchi.

Aliwataka viongozi hao kutumia changamoto na matatizo wanayopelekewa na wananchi kuwabana wenyeviti wa serikali za mitaa, ili kuhakikisha hawarudi mwaka 2014.

“Ndugu zangu wa Kilungule ‘B’ pamoja na changamoto za kisiasa mlizokuwa nazo mmefanikiwa kujenga ofisi za matawi na misingi … zitumieni vizuri, ili tuweze kupata ushindi mkubwa katika chaguzi zinazokuja,” alisema.

Mnyika pia amewakabidhi viongozi wa matawi hayo taarifa za mipango na matumizi ya maendeleo ya jimbo lao ili kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mambo yanayotekelezwa na yasiyotekelezwa na serikali.

pamoja na mambo mengine, Mnyika alitumia fursa hiyo kutoa mwongozo wa kudai Katiba mpya, ili kuhakikisha mwaka 2015 wanapata Katiba itakayowaondolea dhuluma nyakati za uchaguzi mkuu.

Tanzania Daima

Thursday, 20 September 2012

Jaji Mkuu, Othman Chande aahirisha kesi ya rufaa ya Godbless Lema

Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi wao ambaye maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.

Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.

Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).

Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa, umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za CHADEMA ambapo Lema aliongea na wananchi waliokuwa wakimsindikiza na kuwasihi kuwaombea Majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki, “mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi,” alisema Lema.

Katika kesi hiyo, Lema anatetewa na Tundu Lissu, wakati kaka yake, Alute Mughwai, anawatetea walalamikaji.

Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.

Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.

Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.

Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.
 
 
 
 
 
Kamanda lema akiwa nje ya mahakama

Kamanda Lema wakati anaingia Mahakamani leo

Wananchi wa Arusha mjini wakimsikiliza Kamanda Lema kabla ya kwenda mahakamani leo.
 
 
 
 
 
 
 
 

Chadema Wamlima Barua JK

WAMTAKA ACHUKUE HATUA DHIDI YA MAUAJI YA RAIA KINYUME CHAKE SERIKALI INAHUSIKA

 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemwandikia barua Rais Jakaya Kikwete kikimtaka achukue hatua dhidi ya matukio kadhaa ya mauaji ya raia yaliyotokea kwa nyakati tofauti katika mikutano yake ya hadhara kwenye Mikoa ya Singida, Tabora, Arusha, Morogoro, Iringa.
 
Hatua kilichopendeza ni pamoja na kuwawajibisha viongozi wenye dhamana; Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Polisi, IGP Said Mwema; Mkuu wa Operesheni Maalumu Polisi, Paul Chagonja, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.
Barua hiyo ya Septemba 10, mwaka huu iliyoandikwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe baada ya kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho, imemtaka Rais Kikwete kuwafukuza kazi watendaji hao katika Serikali yake kwa kuwa wameshindwa kazi. Kimesema kwamba mauaji mengi miongoni mwa hayo, yametokea bila hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa na kusema kwamba ukimya huo unaweza kutoa picha potofu kwa umma kwamba Serikali yake inaunga mkono au imewatuma polisi au watu wengine waliosababisha mauaji hayo.

Matukio ya vifo ambayo chama hicho kimetaka yachunguzwe ni pamoja na lile la Januari Mosi, mwaka jana mkoani Arusha, Igunga (Novemba, mwaka jana) na Arumeru Mashariki (Aprili, mwaka huu). Mengine ni lile la Iramba lililotokea Julai 14, mwaka huu, Morogoro (Agosti 27, mwaka huu) na Iringa Septemba 2, mwaka huu ambalo hata hivyo, shauri lake limeshafikishwa mahakamani. Kimedai kwamba katika Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Kiongozi wa Kata wa chama hicho, Msafiri Mbwambo alichinjwa huku chanzo cha kifo hicho kikielezwa kuwa ni masuala ya kisiasa.


Pia kilielezea mauaji yaliyotokea katika Kijiji cha Ndago, Wilaya ya Iramba, Singida na kudai kwamba kikundi cha watu kilivamia mkutano wa Chadema kwa mawe na kwamba licha ya polisi kuwapo eneo hilo, hawakuchukua hatua zozote. Chama hicho pia kimekumbusha mauaji ya mfuasi wake mkoani Morogoro, Ally Zona kikisema kifo hicho pia kina utata kwani taarifa ya polisi imesema alikufa kwa kugongwa na kitu kizito wakati chama hicho kikidhani kwamba alipigwa risasi.


Kimesema pamoja na matukio yote hayo, viongozi wote hao hawakuchukuliwa hatua zozote za kuwajibika kwa matukio hayo. Pia Chadema kimeonya kuwa hali hiyo ikiachwa inaweza kujenga dhana potofu kwa wananchi kuwa Jeshi la Polisi liko mikononi mwa CCM na kazi yake ni kulinda masilahi ya chama hicho kwa gharama yoyote ile jambo ambalo Mbowe alisema ikiwa Rais Kikwete atachukua hatua za kinidhamu dhidi ya viongozi hao, atakuwa ameudhihirishia umma kwamba Serikali yake haifumbii macho mauaji yanayofanywa na vyombo vya usalama nchini. Kimemtaka Rais Kikwete kuunda tume ya kijaji au kimahakama kuchunguza vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yanayokihusisha Chadema.


Ikulu yajibu Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue alipoulizwa juu ya barua hiyo alisema haijafika ofisini kwake, huku akisisitiza kuwa kama imeandikwa kwa Rais si lazima ifike kwake.“Sijaiona, ila kama wamemwandikia Rais barua sidhani kama itakuja kwangu. Itakwenda kwake moja kwa moja,” alisema Balozi Sefue. Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye hakutaka kuzungumzia hatua hiyo ya Chadema akisema, “Siwezi kusema chochote kwa kuwa barua yenyewe sijaiona pia ni barua ya Rais.”Kauli ya Bavicha Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limemtaka Rais Kikwete kuunda tume huru yenye wataalamu wa sheria ili kuchunguza mauaji, utekaji, vurugu na unyanyasaji wa wananchi unaotokea kwenye mikutano ya siasa hasa inayokihusisha chama hicho.


Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Morogoro baada ya kikao cha baraza hilo taifa, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche alisema kwamba kama Rais Kikwete atashindwa kufanya hivyo, baraza lake kwa kutambua kuwa matukio mengi ya mauaji yamehusisha vijana, litahamasisha maandamano nchi nzima na kuishtaki Serikali yake.
 
Habari hii imeandikwa na Fidelis Butahe na George Njogopa, Dar na Hamida Sharif, Morogoro. www.mwananchi.co.tz

CHOPA NNE KUONGEZA NGUVU KATIKA AWAMU NYINGINE YA M4C

Ni awamu nyingine ya M4C
Zitashambulia mikoa minne
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinakusudia kuendelea na Operesheni Sangara kwa nguvu kubwa ikiwemo kutumia helkopta nne na kuongeza idadi ya magari katika mikoa mbalimbali nchini kwa lengo la kuyafikia maeneo mengi ambayo miundombinu yake ni mibovu.

Chama hicho kitatumia helikopta hizo wiki mbili zijazo kitakapoendelea na operesheni hiyo yenye kauli mbiu ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) katika Mkoa wa Iringa.

Operesheni hiyo ilitarajiwa kuanza mkoani Iringa Agosti 28, mwaka huu, lakini ilisitishwa baada ya chama hicho kukubaliana na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Said Mwema, kwamba iendelee baada ya kumalizika kwa sensa ya watu na makazi.

Baada ya sensa kumalizika, Chadema kilitangaza kuisitisha operesheni hiyo kufuatia tukio la mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, mkoani Iringa, Daudi Mwangosi kwa bomu wakati polisi wakikabiliana na wa wafuasi wa chama hicho kwenye ufunguzi wa tawi katika kijiji cha Nyololo katika wilaya ya mufindi, mkoani Iringa.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Morogoro jana baada ya kumalizika kwa kikao cha Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), Mwenyekiti wake, John Heche, alisema kuwa operesheni hiyo inatarajia kuanza tena ndani ya wiki mbili zijazo na itanzia mkoani Iringa na kuendelea katika mikoa mingine.

“Kwa taarifa yenu, sasa tutaruka angani na chopa nne kuongeza nguvu Operesheni Sangara, tutaendelea na Mkoa wa Iringa ambako tuliisimamisha kutokana na mauaji ya Mwangosi,” alisema Heche na kuongeza: “Tukitoka hapo tunapiga mikoa mingine.”

Heche alisema lengo la kutumia helikopta hizo nne ni kuwafikia wananchi wengi kuanzia ngazi ya kitongoji ili kuwaeleza mambo mbalimbali, yakiwemo maovu yanayofanyika nchini.

Mwenyekiti huyo wa Bavicha alisema hatua hiyo inatokana na baadhi ya sehemu katika wilaya mbalimbali na mikoa nchini kutofikika kwa njia ya gari kutokana na ubovu wa mindombinu ya barabara ambayo katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru Serikali ya CCM imeshindwa kuiboresha.

Akizungumzia maazimio ya kikao cha kamati ya Utendaji cha Bavicha, alisema kuwa mstakabali wa vijana wa taifa hili hivi sasa unakabiliwa na na changamoto nyingi kutokana na serikali ya CCM kushindwa kusimamia mambo mbalimbali.

Alisema kutokana na hali hiyo, Kamati Tendaji ya Bavicha imeiagiza sekretarieti yake kuunda kikosi kazi au kamati ya kufanya utafiti zaidi ili kujua kwa kina matatizo ya vijana hususani kuanzia masuala ya kuporomoka kwa elimu, ukosefu wa ajira na kutoa ushauri juu ya mstakabali wa taifa baada ya mwaka 2015.

Heche alisema kuwa Bavicha itaendelea kuwaunga mkono walalahoi nchini, wakiwamo wamachinga na matatizo yanayowakabili wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu katika kupata mikopo yao pamoja na kuvifuatilia viwanda ambavyo vilikuwa vikitoa ajira mbalimbali na hivi sasa vimegeuka kuwa mabanda ya mifugo.

Mbali na maazimio hayo, pia baraza hilo limetoa tahadhari kwa vyombo vya dola na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuepusha kauli za vitisho zinazohatarisha amani ya nchi.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bavicha Zanzibar, Sharifa Suleiman, alisema vurugu zote zinazotokea kwenye majukwaa ya kisiasa kwa sehemu kubwa zinatokana na propaganda zinazofanywa na CCM kwa lengo la kuichafua Chadema na kupendekeza kuwa ni muhimu CCM kikaondolewa kwenye orodha ya vyama vya siasa nchini.

“Tumeshuhudia wananchi wakiendelea kunyanyaswa na vyombo vyao vya dola wanavyovilipa kwa kodi zao,” alisema Sharifa.

Akifafanua zaidi alisema vyombo vya dola viondokane na mfumo wa kinyanyasaji wa kujichunguza vyenyewe na kulitaka Jeshi la Polisi kujisafisha kabla wanachi hawajaamka na kukataa kukandamizaji unaofanywa na baadhi ya askari wake bila kuchukuliwa hatua zozote.

Chadema ilianzia Operesheni Sangara katika Mkoa wa Morogoro na ilitarajia kuendelea nayo katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida na Njombe.
CHANZO: NIPASHE

BAVICHA WALIA NA KIKWETE

BARAZA la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo, BAVICHA, limemtaka Rais Jakaya Kikwete na serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuiepusha nchi katika machafuko kwa kuwawajibisha haraka viongozi wa dola katika Wizara ya Mambo ya Ndani kutokana na tuhuma za unyanyasaji, mateso na mauaji kwa raia wasio na hatia endapo wao hawataki kujitoa.

Waliotajwa wajiuzulu au wawajibishwe na Rais kwa maslahi ya umma ni Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emanuel Nchimbi na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Saidi Mwema.

Aidha Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja, kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro, Faustin Shilogile, Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, na wakuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mikoa hiyo wamependekeza washtakiwe.

Akisoma maazimio ya baraza hilo la taifa lililofanyika mjini hapa kwa siku tatu, Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa, John Heche, alisema tayari serikali imeiweka nchi rehani kutokana na kufumbia macho matukio hayo yanayoendelea kufanywa na vyombo vya usalama.

“Mpaka sasa wananchi hawana imani na serikali yao hususan Jeshi la Polisi na haya matukio yameubadilisha ulimwengu jinsi polisi wanavyoendesha unyama kwa raia wasio na hatia kwa visingizio visivyo na maana,” alisema Heche.

Akifafanua juu maazimio 10 yaliyofikiwa na ya baraza hilo, Heche alisema kwa muda mrefu Jeshi la Polisi limekuwa likitumika kama kivuli cha Chama cha Mapinduzi kuficha uovu wake na lenyewe kujificha kwa chama hicho.

“Uone nchi hii inavyokwenda, huyu Kamuhanda aliua watu wanne Songea kumlinda kahamishiwa Iringa nako amefanya hayo hayo mpaka sasa hajakamatwa, huyo Shilogile aliua hapa Morogoro anafunikwafunikwa na hawa wote wamekuwa wakilindwa na makao makuu kupitia mkuu wa operesheni jeshi la polisi Paul Chagonja ambaye anaeneza uongo kwa umma kuwalinda polisi wenzie,” aliongeza.

Katika maazimio hayo likiwemo la kuwataka kujiuzulu, kuwajibishwa au kufunguliwa kosa la mauaji kwa mantiki ya ‘Common intention’ viongozi hao, BAVICHA pia lilimtaka Rais Kikwete kuunda tume huru ya kiuchunguzi ya kimahakama katika makosa yote yaliyotokea Arusha, Arumeru, Igunga, Ndago-Singida, Morogoro na Iringa.

Aidha baraza hilo linakusudia kuunda kikosi kitakachotafiti matatizo ya vijana likiwemo suala la elimu duni na ukosefu wa ajira na kutoa ushauri juu ya mustakabli wa taifa baada ya 2015, kuendelea kuwaunga mkono walalahoi nchini wakiwemo machinga, na imelaani CCM kuwatumia vijana katika mafunzo ya kijasusi kwani yanalenga kulichafua taifa.

Mbali na maazimio hayo pia baraza hili limetoa tahadhari kwa vyombo vya dola na Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa kuepusha kauli za vitisho zinazohatarisha amani ya nchi huku wakimshauri kuifuta CCM kwa kufundisha ujasusi.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa BAVICHA Sharifa Suleiman alisema baraza limepitia na kuchambua kwa kina mustakabali wa kisiasa, vijana na sintofahamu iliyopo na inayozidi kudhihirika kuwa uongozi uliopo umeshindwa kuongoza hasa katika kusimamia rasilimali za nchi kwa faida ya Watanzania.

Tanzania Daima

Tuesday, 18 September 2012

"Ni kuchagua baina ya kuwa kama Uingereza ama kuwa kama Zaire/Kongo." Mistari kutoka kwa Jenerali Ulimwengu

NI dhahiri kwamba nchi inaweza kuwa ndogo lakini watu wake wakawa wakubwa, wakati ambapo nchi inaweza kuwa kubwa na watu wake wakawa wadogo. Hapa nazungumzia nchi yenye ukubwa wa ardhi na ukubwa wa idadi ya watu. Wakati mwingine sifa hizi zinaweza pia kuambatana na nchi kuwa na rasilimali kubwa na nyingi za kutosha.
 
Ziko nchi kubwa kwa maana ya ukubwa wa ardhi na watu na pia rasilimali maridhawa, lakini ambazo watu wake wamebakia kuwa wadogo, na mataifa yaliyoundwa na watu hao yakawa ni madogo pia. Hizi ni jamii na nchi za watu wapuuzi. Nchi ambazo kwa ukubwa wa maili za mraba na ukubwa wa idadi ya watu ni ndogo lakini zikawa na watu wakubwa na mataifa yake yakawa makubwa ni nchi za watu walio makini.

Napenda kuvitaja vielelezo kadhaa vinavyodhirisha kiwango cha juu cha upuuzi ndani ya jamii au nchi ambayo inakuwa kubwa kwa eneo la maili za mraba, wingi wa watu na rasilimali kubwa. Mojawapo ya vielelezo vikubwa vya upuuzi unaoweza kufanywa na jamii au nchi ni pale nchi au jamii inaposhindwa kutumia rasilimali zake kwa manufaa ya watu wake na badala yake ikaziruhusu zikaendelea kuwanufaisha wageni wakati watu wake wanaendelea kudhalilika.

Aina hii ya nchi kimsingi ni nchi iliyokosa uongozi na ikawa inaendeshwa na watawala ambao ama hawana uwezo ama hawana utashi wa kuwaongoza watu wao kuelekea katika maendeleo ya kweli. Mara nyingi hawa ni watawala wanaotawaliwa na uroho wa utajiri binafsi na ambao muda wao mwingi watakuwa katika shughuli za kujikusanyia mali wasiweze kufikia masuala magumu ya maendeleo ya watu wao.

Aghalabu pia watawala wa aina hii watakuwa ni wapagazi wa mabwana wao kutoka nje, hawa wakiwa ni watu binafsi, serikali, makamupuni ya biashara na asasi za kiulinzi na kijasusi. Watawala wa aina hii wanawatumikia wageni na hawana haya kuonyesha hali hiyo. Ndio wale ambao kila wakishutumiwa kwa hili au lile wanakuwa wepesi kusema, “Mbona huko nje wanatushangilia?” Kana kwamba “huko nje’ ndiko kulikowachagua.

Mwisho wa siku watawala kama hawa hupoteza haiba (kama waliwahi kuwa nayo), huonekana zaidi wakijipendekeza kwa wageni, na huanza pole pole kuwaogopa watu wao kwa sababu hawana majibu kw maswali wanayoulizwa na watu wao ambao hawawezi kuelewa ufukukara wao unasababishwa na nin katika mazingira ya utajiri mkubwa. Na wala hawawezi kuelewa ubadhirifu unaofanywa na watawala ambao maelezo yao ya siku zote ni hali ngumu ya uchumi duniani.

Hawa ndio watawala wa nchi kama Zaire/Kongo niliowajadili majuzi, na ndio watawala wa nchi kama Nigeria. Zote hizi mbili ni nchi kubwa zenye watu wadogo zinaotawaliwa na watawala walafi. Haziwezi hata kidogo kuwa mataifa makubwa hata zingekuwa na utajiri mkubwa kiasi gani.

Nje ya bara la Afrika, ni nchi kama Urusi ambayo baada ya kusambaratika kwa himaya ya Sovieti (ambayo nayo ilikwisha kupoteza pumzi mapema) imekuwa ikijikokota chini kabisa ya utajiri ilio nao na uwezo wa watu wake. Leo Warusi ni watu wadogo, na taifa lao ni dogo likilinganishwa na ‘potensho’ yake. (Vijana wa Kenya waliimba: “Nchi ya kitu kidogo, nchi ya watu wadogo”).
Upande mwingine tunaona mataifa makubwa yaliyojengeka ndani ya nchi ndogo, kama Botswana na Mauritius, nchi zenye rasilimali kidogo lakini zenye uongozi makini ambazo zimeweza kuwafanya watu wake wawe wakubwa na watambulike hivyo duniani.

Katika historia ya dunia ya karne kadhaa zilizopita tunajifunza kwamba ‘kijinchi’ kama Uingereza, ambacho hakikuwa na lo lote wakati huo, kikiwa kimefungwa katika kisiwa ambacho kwa nusu ya mwaka kimeganda na barafu, kiliweza kutawala nusu ya dunia ya wakati ule na kuwaweka mamilioni ya wanadamu chini ya himaya yake kutoka mashariki hadi magharibi, kaskazini hadi kusini.
Ni jambo gani liliifanya Uingereza iweze kuitawala dunia, kutawala Bara Hindi pamoja na watu wengi wale, tena wenye mapokeo na utamaduni wa fahari? Ni nguvu ya kujiamini, kuamini katika uwezo mkubwa wa jamii na uongozi wake na kuamini katika uwezo usiotishika wala kutikisika mbele ya adui au mpinzani ye yote.

Imani hii katika uwezo wa Uingereza ilipandikizwa akilini na mioyoni mwa watoto wa Uingereza tangu wakiwa ‘nkeremeke’ (neno la Kihaya linalomaanisha kichanga) na imani ambayo walikuwa nayo ikawa ni silaha kubwa kila walikokwenda kupora nchi za watu wengine ili kuiletea fahari himaya ya Uingereza.
Hawakuendekeza watawala wala rushwa na wasaliti wa watu wao, na angalau mara moja mfalme wao alipodhihirika kutaka kuwakandamiza walizua uasi na wakamkamata na kumkata kichwa. Katika msukumo wa kutafuta fahari ya Uingereza hawakuvumilia upuuzi.

Mzee mmoja wa Uingereza aliyewahi kufanya kazi kama mtawala wa kikoloni nchini Tanganyika aliniambia kuwa siku ya kwanza shuleni walikusanywa kwenye gwaride la shule nzima na mkuu wa shule akawaambia: ‘Nyie watoto mna bahati kwani mmezaliwa mkiwa Waingereza. Hiyo ina maana mmeshinda bahati nasibu ya kwanza katika maisha yenu.”

Nani anaweza kuwaambia watoto wa Tanzania kitu kama hicho leo hii? Katika mazingira mengi watoto wanaweza hata kumzomea kwa sababu hawaoni ni nini hasa kiwafanye waone fahari ya kuwa Watanzania, watu wenye mashaka katika kila idara ya maisha yao, wanaoongozwa na watawala ambao wanaelekea bado wanatafuta kuelewa ni nini hasa maana ya uongozi?

Jamii au nchi inakuwa ya kipuuzi iwapo ina kila aina ya rasilimali lakini rasilimali hizo haziisaidii jamii wala nchi kuendelea wala kuwa jamii au nchi ya furaha. Furaha ndani ya jamii si lazima itokane na maendeleo makubwa ya kiuchumi na ujenzi wa vitu kama barabara na majumba. Hivi ni muhimu, lakini si kila kitu. Zipo jamii duniani ambazo kwa vigezo hivi zinaitwa jamii masikini, lakini viwango vyake vya furaha viko juu sana.

Hizi ni jamii ambazo zimeridhika na hali ya maisha kwa sababu zimeweza kujenga utangamano kati ya rasilimali zilizopo na mafanikio ya kimaisha ya watu wake. Mathalan, jamii inaingiza kipato cha shilingi kumi, kila mwanajamii analijua hilo, halafu jamii inanufaika kwa kiwango cha shilingi kumi, na kila mwanajamii analijua na kulielewa hilo, na wanajamii wote, isipokuwa mwendawazimu, wanaridhika.

Jamii inajihatarisha yenyewe iwapo itafanya kinyume cha hilo, iwapo, mathalan, itaingiza kipato cha shilingi kumi kisha ikaruhusu shilingi moja tu itumike kwa manufaa ya jamii halafu jamii isijue shilingi tisa zilizobaki zimetumika vipi. Hata kama hakuna wizi au ubadhirifu katika matumizi bado misingi ya vita itakuwa imekwisha kujengwa kutokana na nakisi ya taarifa, uwazi, uelewa na maridhiano.

Maridhiano ni tunda la maelewano na maelewano ni tunda la kueleweshana katika uwazi. Uwazi unapopungua na sehemu ya jamii ikahisi kwamba inadhulumiwa au haitendewi haki unakuwa ndio mwanzo wa chokochoko na mfarakano.

Uwezo wa kuchagua umo ndani yetu. Tunaweza kuchagua kuwa nchi kubwa kwa maana ya eneo la maili za mraba na idadi kubwa ya watu (na rasilimali nyingi na kubwa) lakini papo hapo tukawa taifa la wapuuzi, tukajulikana hivyo duniani, au tukachagua kuwa taifa dogo kwa vigezo vya ukubwa wa ardhi, idadi ya watu na rasilimali lakini tukatumia rasilimali hizo ndogo, udogo wa idadi ya watu wetu na udogo wa eneo la mraba la nchi yetu kuwa (na kutambulika kama) taifa kubwa.

Ni kuchagua baina ya kuwa kama Uingereza ama kuwa kama Zaire/Kongo
 
Jenerali Ulimwengu, Rai ya Ulimwengu, Raia mwema, Toleo la 257, 5 Sep 2012

 

MBUNGE WENJE AUTEKA MKUTANO WA PINDA

Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Hezekiah Wenje, jana aliuteka mkutano uliopangwa kuhutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambapo wananchi waliohudhuria walimshangilia zaidi yeye (Wenje) huku wakinyoosha vidole viwili ambayo ni alama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Hali hiyo ilijiri jana saa 11:00 baada ya msafara wa Waziri Mkuu kuingia katika viwanja vya Sahara huku Wenje akiwa miongoni mwa waliofuatana na Pinda.

Baada ya Pinda kuteremka kwenye gari na kuanza kuelekea kwenye meza kuu huku akisalimiana na baadhi ya wananchi, sehemu kubwa ya umati uliokuwepo walikuwa wakionyesha ishara ya vidole viwili na mara walipomuona Wenje walilipuka kwa shangwe ambapo Mbunge huyo machachari naye aliwanyooshea ishara ya vidole viwili.

Kama vile haitoshi baada ya Waziri Mkuu na viongozi wa mkoa wa Mwanza aliokuwa amefuatana nao kuketi vitini, ndipo Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, alisimama kwa ajili ya kufanya utambulisho na alianza kwa kumweleza Pinda kuwa hizo ndizo harakati za miji mikubwa.

Wakati Konisaga akisema hivyo, wananchi waliendelea kushangilia, hali iliyomfanya adai kuwa wanamshangilia yeye (Konisaga) kwa sababu ndiye mtawala wa eneo hilo, lakini wananchi walionekana kuguna kwa sauti kama ishara ya kutokubaliana naye.

“Hayo makofi mnanishangilia mimi, kwa sababu bila mimi hakuna mkutano,” alisema Konisaga na kupokelewa na sauti za wananchi walionekana kupingana naye wakisema weweeee! Katika utambulisho, Konisaga alianza kwa kumtambulisha Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, lakini wananchi walionekana kupinga hatua hiyo ndipo Konisaga akawaambia bila yeye (Kabwe) hakuna maendeleo Mwanza.

Hatimaye Konisaga alimtambulisha Wenje ambaye alisimama kuelekea jukwaani huku akishangiliwa kwa nguvu na wananchi ambao walikuwa wakimshangilia kwa kuimba “mbunge, mbunge, mbunge”.

Alipofika jukwaani na kupewa kipaza sauti, Wenje alianza kwa kusema: “Mheshimiwa Waziri Mkuu, hili ndilo Jiji la Mwanza. Kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita sijawahi kuona nguo za kijana uwanjani hapa.”

Kauli yake ilizididha mlipuko wa sauti za wananchi wakimshangilia na ndipo alianza kumweleza Waziri Mkuu kwamba Jiji la Mwanza lina malalamiko mengi ya wananchi kuhusu migogoro ya ardhi.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, Jiji la Mwanza lina malalamiko mengi ya ardhi. Nimesema sana ndani ya Bunge, lakini mnanijibu kisanii. Nimemweleza na Waziri wa Ardhi kwamba wanaoteseka sio Chadema peke yao kwani hata wana-CCM nao wana malalamiko vilevile,” alisema.

Wenje ambaye alikuwa amepewa nafasi ya kusalimia tu, aliongeza kuwa ni matumaini yake kwamba ujio wa Waziri Mkuu katika mkoa wa Mwanza utaleta ufumbuzi wa migogoro iliyokithiri katika sekta ya ardhi.

CHANZO: NIPASHE

PINDA AZOMEWA MWANZA, MKUTANO WAKE WANUSURIWA NA MBUNGE WENJE WA CHADEMA

VIJANA MWANZA WAIMBA ‘PEOPLE’S POWER, HATUITAKI CCM’

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, jana alijikuta katika wakati mgumu baada ya kushindwa kuhutubia maelfu ya wakazi wa Wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza kwa muda kutokana na wananchi wengi kumzomea.

Kiongozi huyo alikumbana na kisanga hicho cha aina yake akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Clement Mabina pamoja na Mkuu wa Mkoa huo, Mhandisi Evarist Welle Ndikilo.

Pinda na viongozi hao, walikumbana na zomeazomea hiyo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Sahara jijini hapa, ikiwa ni hitimisho la ziara ya Waziri Mkuu huyo ya siku saba mkoani Mwanza.

Chanzo cha Pinda na viongozi hao kuzomewa mkutanoni hapo, ilitokana na kile kilichoonekana kuwepo kwa kero nyingi zilizodaiwa kushindwa kupatiwa ufumbuzi na Serikali ya CCM chini ya Rais Jakaya Kikwete.

Kitendo hicho cha wananchi kilimlazimisha Pinda kushindwa kuhutubia kwa muda, huku akionekana kujawa jazba.

Sababu nyingine ya wananchi kuzomea, ni hatua ya Pinda kuwaambia wananchi hao watoke mjini waende vijijini wakalime waachane na mambo ya upinzani wa kisiasa.

Pinda alitoa kauli hiyo baada ya kundi la vijana mkutanoni hapo kuonesha alama ya V, bendera ya CHADEMA na nyimbo za Peoples, Power.

Kwa mazingira hayo, askari wa polisi wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), waliokuwa na silaha nzito za kivita aina ya SMG, mabomu na marungu waliokuwepo mkutanoni hapo, walianza kuwatishia kuwapiga wananchi hao kwa lengo la kumlinda kiongozi huyo.

Baada ya kuzidi zomeazomea hiyo, Waziri Mkuu, Pinda alilazimika kumuita mbunge wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), aliyekuwa meza kuu, kisha kusema: "Nyamazeni basi!. Wenje...hii ndiyo serikali ya siku chache zijazo. Kwa namna hii naona hamuwezi, maana itakuwa ni vurugu asubuhi hadi jioni". Akazomewa kisha wakaimba hatutaki CCM, hatutaki CCM. .

Baada ya kuona hivyo, Pinda akacheka na kusema: "Hahahaaaaa, hata mkiimba peoples power, CCM ndiyo inayowaongoza". Akazomewa tena kisha Pinda akashindwa kuendelea kuzungumza jukwaani.

Akahutubia mkutanoni hapo, Pinda aliwataka wananchi hao waache ushabiki wa kisiasa, na kwamba halmashauri ya jiji la Mwanza inayoongozwa na CHADEMA, ndiyo itapaswa kulaumiwa kama itashindwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi wake.

"Hapa jiji la Mwanza linaongozwa na CHADEMA. Meya wa CHADEMA, mwenyekiti wa Mipango miji wa CHADEMA, Naibu Meya ni wa CHADEMA. Lakini kama wameshindwa kuweka mipango mikakati ya kuwasaidia tutasema hawafai," alisema kisha akazomewa kwa mara nyingine.

Baada ya zomeazomea hiyo kuonekana kumwelemea Waziri Mkuu huyo, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Ndikilo alilazimika kuingilia kati kwa kusema: "Wanaozomea tunawafahamu, na tunawafahamu waliowaleta hapa ili mje kufanya nini". Akazomewa.

Hata hivyo, baada ya hali kutulia kidogo, Pinda aliendelea kuhutubia huku akiwataka wananchi wa jiji la Mwanza waondoke mjini waende vijijini wakalime, jambo lililoonekana pia kuwakasirisha wananchi wengi kisha kumzomea tena.

Ingawa Pinda alilazimika kutumia muda mfupi kutoa hotuba yake, aliwaomba wana Mwanza washirikiane kuleta maendeleo yao, na kwamba iwapo tatizo ni Mkurugenzi wa jiji suala hilo litaangaliwa.

Aliwaomba wadumishe amani iliyopo hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kushirikiana na Serikali kupambana na vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, ili kuweza kuzua samaki wadogo wasivuliwe kisha kuharibu mazalia ya rasilimali hiyo.

"Jambo jingine ninalotaka kuwaeleza hapa leo ni hili la uvuvi haramu. Samaki ndani ya Ziwa Victoria wameisha...na hii ni kwa sababu ya uvuvi usiozingatia sheria. Tushirikianeni kupambana na vitendo hivi", alisema Pinda kisha akazomewa tepa.

Tanzania Daima

BAVICHA TAIFA WAKUTANA MOROGORO KUPANGA MIKAKATI YA KUIMARISHA CHAMAJohn Heche , Septemba 17, 2012 alifungua Kikao cha Kamati ya Utendaji ya Bavicha kilichohudhuriwa na wajumbe kadhaa kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani.Kikao hicho kilipanga kujadili ajenda mbalimbali za Vijana na baadaye kufikia kutoa tamko la pampoja kuhusiana na masuala ya kisiasa, kijamii na kiuchumi.Hata hivyo katika Kikao hicho , Bavicha kupitia Mwenyekiti wake wa Taifa , walimkaribisha Mwandishi wa Habari na Mtangazani wa zamani wa TBC, Jerry Muro ili aweze kuwasalimia wa wajumbe wa Baraza hilo walioanza kukutana tangu Septamba 14 hadi 18, mwaka huu.Katika salaamu zake , Muro alisema, yenye ni mwanaharakati na mtu anayependa kusema ukweli, hivyo kwake mtu kama huyo ni lazima amuunge mkono kama ilivyo kwa vijana wa Bavicha wanavyosimamia kusema ukweli na kuamua kuwaunga mkono kwa hilo

Monday, 17 September 2012

Mheshimiwa Ndesamburo akutana na Mwenyekiti Wa Chadema UK


CHADEMA kuanika ‘siri’ ya mauaji

VIJANA WAKE WASEMA SASA YATOSHA
BARAZA la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) leo linatarajiwa kuanika hadharani ukweli wa mauaji ya raia yanayodaiwa kufanywa na vyombo vya serikali katika mikoa kadhaa hapa nchini.

Kamati ya Utendaji ya BAVICHA, inayokutana mjini Morogoro, imesema itaweka wazi sintofahamu ya mauaji hayo yenye mwelekeo wa kisiasa bila uchunguzi huru kufanyika ili hatua stahili zichukuliwe kwa wahusika.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, BAVICHA imesema kuwa wamelazimika kufanya hivyo kwa kuwa inaamini haki ya kuishi hata kama ni ya raia mmoja, ina thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote.

Bazara hilo limesema kuwa mauaji ya kada wao Mbwana Masudi, ambaye alitekwa na kuteswa mara baada ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Igunda alikutwa ameuawa kikatili na watu ambao wanaaminika kuwa wafuasi wa CCM.

Wamesema hata baada ya uchaguzi wa Arumeru, kulikuwa na matukio mawili ya mauaji ambayo yote kwa namna moja yamehusishwa na siasa. Tukio la kwanza ni lile ambalo vijana watano walikutwa wameuawa huko Chekeleni, Arumeru, wakati tukio la pili ni lile lililomhusisha kiongozi wa CHADEMA, kata ya Arumeru, Msafiri Mbwambo, ambaye aliuawa kwa kuchinjwa.

Pamoja na kueleza vifo vya wanachama wake, BAVICHA walisema hawafurahishwi na kifo cha yeyote na ndiyo maana watatoa tamko hata la mauaji ya kijana katika kijiji cha Ndago, Iramba, mkoani Singida, aliyetajwa kuwa kiongozi wa UVCCM aliyekutwa amekufa katika mazingira ya kutatanisha ambayo yanahusishwa na siasa.

“Mauaji ya namna hiyohiyo yamefanyikwa hivi karibuni katika mkoa wa Morogoro ambako kijana mmoja, Ali Zona, aliuawa na polisi wakati jeshi hilo lilipovuruga mapokezi ya viongozi wa CHADEMA kwenda kwenye mkutano mkubwa wa hadhara.

Wamesema hali hiyohiyo imejirudia karibuni kabisa katika kijiji cha Nyololo, Iringa, ambapo mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daud Mwangosi, aliuawa kikatili na kinyama na Jeshi la Polisi kwa kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu.

“Kwa namna yoyote ile Kamati ya Utendaji ya BAVICHA haiwezi kufumbia macho mauaji haya ambayo kwa kweli yana nia ya kudhibiti kasi ya mabadiliko ambayo watawala wanaiona kuwa inazidi kupamba moto.

Katika mauaji haya, hakuna hatua zozote za makusudi zilizochuliwa dhidi ya wale waliohusika na kikubwa serikali kupitia vyombo vyake imekuwa ikifanya mzaha katika kushughulikia jambo hili. Mauaji haya yanayotekelezwa na jeshi la polisi kwa amri za serikali ya CCM yamekuwa na dhamira moja tu ya kutaka kuupotosha umma kuwa CHADEMA ni chama cha fujo,” wamesema.

Waituhumu CCM kufadhili vijana wake

Katika hatua nyingine BAVICHA imekishukia Chama cha Mapinduzi kwa madai ya kufadhili vijana wake na kuwaweka kwenye makambi ambako wanafundishwa mbinu haramu za kudhuru raia wenzao ambao wanaonekana kuipinga hadharani.

Vijana hao wamesema wanao ushahidi wa kutosha unaodhihirisha kuwa mafunzo hayo yanatolewa na baadhi ya vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi, kama ilivyofanywa kwenye makambi maeneo ya Irmaba, Singida, na Tabora wakati wa uchaguzi mdogo wa Igunga.

Aidha CCM imeendelea kutumia vijana kwa kuwakodi kutoka sehemu mbalimbali na kuwapeleka sehemu nyingine ya nchi kwa lengo la kutibua na kufanya fujo kwenye mikutano ya CHADEMA. Hali hii inathibitishwa na tukio la Ndago, mkoani Singida.

Askofu Mkuu Mtega avunja ukimya

Huko mjini Songea, mwandishi wetu Julius Konala, anaripoti kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Mhashamu Norbert Mtega amevitaka vyombo vya dola kuacha mchezo wa kutumia silaha kali hovyohovyo na kuchochea machafuko yanayowaumiza watu wasio na hatia.

Mhashamu Mtega alitoa kauli hiyo jana wakati wa sherehe za shirika la Mabinti wa Maria Imaculete DMI, na kuonya kuwa machafuko yanayozikumba nchi nyingi duniani, yalianza kwa mtindo unaoonekana kwa sasa hapa nchini.

Askofu Mtega bila kutaja tukio lolote, alisema madhara yanayoanza kuonekana nchini yamewagusa zaidi kina mama na watoto ambao hawana uwezo wa kujitetea na kuwafanya waangamie bila sababu za msingi.

“Nawaambieni kama tutaachilia mambo haya ya kutumia silaha hovyohovyo yakaendelea kwa kweli tutakuwa tunatafuta machafuko ambayo yatawaumiza watu wasiyo na hatia kabisa,” alisema.

Kauli ya Askofu Mtega inakuja siku chache baada ya kutokea kwa mauaji ya kikatili ya mwandishi wa habari wa kituo cha Runinga cha Channel Ten, Daud Mwangosi, mkoani Iringa, baada ya kupigwa bomu na askari polisi.

Mauaji ya Mwangosi ambayo yalitikisa nchi, yalitokea baada ya askari polisi kuvamia shughuli za ufunguzi wa ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika kijiji cha Nyololo, mkoani Iringa.

Hivi sasa, tume na kamati kadhaa zimeundwa kuchunguza sababu za mauaji hayo, ambapo jeshi la polisi limemfikisha mahakamani askari anayedaiwa kumuua mwandishi huyo wa habari.

Tanzania Daima

Chadema UK Ndani ya Milton Keynes

DAR NI SISI - VIDEO MAISHA YA WANADAR HATA BAADA YA MIAKA50 YA UHURU