Sunday 30 December 2012

CHADEMA M4C-UK HATULALI MPAKA KIELEWEKE
                               
NDUGU MAKAMANDA!!!

NI BUSARA TUPONGEZANE NA KUMSHUKURU MUNGU KWA KUTUJALIA KUVUKA MWAKA 2012 NA KUANZA MWAKA 2013, TUKIWA NA HALI NZURI KIAFYA NA KTK HARAKATI ZA KUMKOMBOA MTANZANIA KIFIKRA.

TUNAJIVUNA KUMALIZA MWAKA KWA KISHINDO KWANI TUMEWEZA KUBAINI NA KUMWAJIBISHA VILIVYO KILA ALIYEFANYA KINYUME NA MATAKWA YA M4C NDANI YA CHADEMA KTK MAANDALIZI YA KUCHUKUA DOLA

NAFARIJIKA KUWAMBIA KWAMBA CHADEMA KUCHUKUA DOLA SI NDOTO TENA, BALI ITAKUWA. HIVYO TUNAWASHAULI KWA KUWAHIMIZA CCM WASIGHARIMIKE KWA KUTUMIA RASILIMALI ZETU NYINGI KUDHOOFISHA HARAKATI ZA UMMA WA WATANZANIA ZINAZOFANYIKA KUPITIA CHADEMA

NAPENDA NIWATIE MOYO KWAMBA, ZAIDI YA SISI (CHADEMA) KUTABILI USHINDI IFIKAPO MWAKA 2015, PIA UMMA TUNAOUPIGANIA UNAJITABILIA USHINDI MKUBWA DHIDI YA CCM LICHA YA PROPAGANDA CHAFU NA NJAMA NYINGINE POTOFU WANAZOZIFANYA KUPITIA VYOMBO VYA DOLA.

TUNAPENDA IELEWEKE KWAMBA MWAKA 2013 TUTAJIPANGA KAMA TAWI LA SERIKALI TARAJIWA YA CHADEMA. KWAHIYO, M4C-UK ITAKUWA KIMKAKATI ZAIDI KULIKO HAMASA. HIVYO TUMENUWIA KUWA NA VIONGOZI SAHIHI WENYE MAONO, WITO, FIKRA SAFI, UTU, NIDHAMU, NA NIA YA MAENDELEO MBADALA KWA WATANZANIA. KWA MANTIKI HII, TUNAKUOMBA WEWE BINAFSI UJIANDAE KUWANIA UONGOZI ILI UTULETEE NJOZI MPYA, ZITAKAZOTUVUSHA NGAMBO ILE  YENYE TANZANIA MPYA TUNAYOITAKA.

MWISHO WA YOTE NATUMIA FURSA HII KUTOA SHUKRANI ZA DHATI KWA UONGOZI WA MUDA NA BAADHI YENU MLIOJITOLEA KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA TAWI LETU LINASONGA MBELE. NAWATAKIA MWAKA MPYA WENYE MAFANIKIO MAKUBWA


MUNGU IBARIKI CHADEMA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
Piipooooooooooz!!!!

IMETOLEWA NA KURUGENZI YA MWASILIANO NA MAHUSIANO YA CHADEMA-UK

Wednesday 12 December 2012


BREAKING NEWS!!!!!
Mwenyekiti wa CHADEMA UK Mr Christopher Lukosi amevuliwa madaraka na kusitishwa uanachama.
Ikiwa ni takribani miezi minne tangu tawi la CHADEMA UK lifunguliwe rasmi na Mr Godbless Lema, kumekuwepo na maendeleo makubwa ya ujenzi wa tawi hili lakini vile vile kumekuwepo na changa moto mbali mbali kutokana na uelewa wa watu ktk dhana nzima ya M4C. M4C ikiwa na maana ya Movement for Change, ni sharti mtu yeyote anayeingia ktk movement hii kwenye ngazi ya uongozi aelewe haya machache ya msingi:
1)   Kwanza aone matatizo yanayomgusa yeye na jamii yake
2)   Ajue na kutambua fika chimbuko la matatizo haya
3)   Awe tayari kuwa kiini cha mabadiliko ya kweli anayoyataka kwa jamii
4)   Aweze kutoa ufumbuzi kwa kukemea maovu, kuelimisha na hata yeye binafsi kuelimika
5)   Ili afanikiwe ktk kipengele cha (4) ni sharti ajitambue yeye binafsi ya kwamba ni:
i)            Lazima awe safi na mwenye sifa za kukemea waovu
ii)           Aweke maslahi ya jamii mbele na si yake binafsi
iii)         Awe na sifa za uongozi zinazotakiwa, nidhamu ikiwa nambari moja ktk orodha.
iv)         Awe na msimamo wa kiitikadi
Kwa hiyo, uongozi wa CHADEMA UK kwa baraka za watetezi wa haki ya kweli (CHADEMA TZ) unawatangazia umma watanzania kokote mlipo kwamba kuanzia leo tarehe 12/12/12, Mr Christopher Lukosi amevuliwa rasmi uongozi na amesitishwa uanachama kutokana na kutokidhi mengi ya yaliyotajwa hapo juu.
Uongozi wa CHADEMA UK unamshukuru sana kwa mchango na ushirikiano wake mkubwa kwa kipindi ambacho matundu ya chujio yalikuwa makubwa. Tutaendelea kumkumbuka na hata kutumia misemo yake yenye maana nzito kwa jamii ya kitanzania, kama vile: -
i)            Sisi sote ni ndugu, tatizo ni CCM
ii)           Kila kwenye msafara wa mamba na kenge wamo
Uongozi unamwakikishia Mr Christopher Lukosi kwamba mamba wote wa CHADEMA UK kwa kushirikiana na wote wenye kuelewa mageuzi ya kweli, tutaliondoa tatizo ifikapo 2015. Tunamtakia kila la kheli katika maisha na ni imani yetu tutaendelea kuwa ndugu yake baada ya tatizo kutatuliwa !!!!.
“We fail in most of our endeavours because we too often underestimate People’s Power” [M4C UK, 2012]

Friday 23 November 2012


  
MKUTATANO WA CHADEMA UK !!!!
Uongozi wa muda wa CHADEMA UK unapenda kuwakumbusha wana kamati wote kwamba kutakuwa mkutano kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi wa kudumu Tarehe 24th November 2012 Jumamosi saa kumi na moja (17:00pm) jioni karibu na Barking Station...Pahala pa mkutano ni pale pale.

Saturday 6 October 2012

Uzinduzi wa kampeni za chadema kata ya daraja II



KWA HABARI ZAIDI NA MATUKIO YANAYOENDELEA MKUTANONI TEMBELEA:

Wauaji wa Kada wa CHADEMA watoroka

POLISI WAHAHA KUFICHA UKWELI, WATOA DAU LA MIL. 5/-
WASHTAKIWA wawili waliompora askari polisi bunduki wakiwa chini ya ulinzi katika mahakama ya mkoa wa Arusha na kutoroka kusikojulikana, katika mazingira ya kutatanisha imebainika kuwa ni wale wanaokabiliwa na tuhuma ya mauaji ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kata ya Usa River, Msafiri Mbwambo.
Washtakiwa hao Samweli Mtinange maarufu kama Samu na Mohamed Shaban Limu walitoroka juzi majira ya saa 7:30 mchana wakati wakitolewa kwenye chumba cha mahabusu mahakamani wakipelekwa kwenye karandinga la polisi kwa ajili kurudishwa rumande kwenye gereza la mkoa, Kisongo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Liberatus Sabas, alithibitisha kutoroka kwa washtakiwa hao wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji namba 184/2012, lakini akakanusha kuporwa bunduki na silaha zaidi ya 30 kwa askari polisi aliyekuwa akiwalinda.
Tukio hilo limezua hofu kubwa na kuzusha tuhuma kuwa limepangwa kiufundi na baadhi ya watu, kwa nia mahsusi za kisiasa hasa ikizingatiwa kutokea kwa tukio jingine baya la mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, mkoani Iringa mwanzoni mwa mwezi uliopita.
Wasiwasi huo umekuja kutokana na mazingira ya tukio hilo, ambalo wadadisi wa mambo wanatia shaka juu ya kutokuwepo kwa mikakati imara iliyosukwa kufanikisha utorokaji huo.
Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imedai kupokea kwa mshtuko na tahadhari kubwa, kitendo cha watuhumiwa wawili wa mauaji hayo, kutoroka mbele ya askari polisi wenye silaha, baada ya kumnyang’anya bunduki mmoja wa askari waliokuwa lindo kwenye eneo la mahakama ya wilaya.
Aidha kurugenzi pia imepokea kwa tahadhari kubwa taarifa kuwa Kamanda wa Polisi (RPC), mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, pamoja na kukiri kuwa waliokimbia mbele ya polisi kwa kumnyang’anya askari silaha ni watuhumiwa wa mauaji ya Mbwambo, aligoma kutaja jina la askari aliyenyang’anywa bunduki na hata majina ya wenzake waliokuwa lindo hapo mahakamani.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Rwakatale, alisema tukio hilo sasa limekifanya chama hicho kianze kuweka mkazo kwenye kuunganisha ‘nukta’ katika matukio ya namna hii na limezidi kudhihirisha pasi na shaka yoyote umuhimu wa kuundwa kwa chombo huru cha uchunguzi wa mauaji yenye utata, yanayohusishwa na siasa, mojawapo likiwa ni tukio la mauaji ya Mbwambo.
Rwakatale amelitaka Jeshi la Polisi kutoa maelezo ya kutosha yatakayoendana na uwajibikaji, unaopaswa kufuatiwa na hatua za kisheria, ili kuweza kujinasua kwenye kashfa hii ya juzi Arusha, ambapo sasa inatafsiriwa kuwa jeshi hilo limehusika kufanya ‘mchezo’ mwingine kwa nia ama ya kutaka kuficha mtandao wa mauaji hasa ya kisiasa au kuficha ushahidi muhimu wa masuala ambayo ama yamebainika kwenye mahojiano au ambayo yangebainika mahakamani, ikizingatiwa kuwa baadhi ya watuhumiwa wa kesi hiyo ni viongozi wa CCM.
“Kitendo cha RPC Sabas kukanusha askari wake kunyang’anywa bunduki, ambayo baadaye iliokotwa ikiwa imetelekezwa, ni dalili za mwendelezo wa tabia ya jeshi hilo, kupitia maofisa wake waandamizi, kujitokeza kuficha ukweli na kufanya propaganda, kwa kila tukio ambalo jeshi hilo linapaswa kuwajibika kwa makosa linayofanya”
“Itakumbukwa pia katika barua ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Mheshimiwa Freeman Mbowe kwenda kwa Rais, chama kilimtaka Rais kuunda Tume ya Kijaji/ Kimahakama ya uchunguzi wa vifo vilivyotokea katika mikusanyiko, mikutano, maandamano au mazingira ya kisiasa yaliyohusisha CHADEMA. Vifo hivi ni vile vilivyotokea Arusha (05/01/2011), Igunga (Novemba 2011), Arumeru Mashariki (Aprili 2012), Iramba (Julai 14, 2012), Morogoro (27/08/2012) na Iringa (02/09/2012),” imesema taarifa hiyo.
CHADEMA imesema kuendelea kutokea kwa masuala yenye utata katika usalama kumeonyesha kuwa serikali ya CCM inazidi kukomaza mfumo wa kulindana na kutaka kuficha masuala fulani fulani, hasa katika matendo ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi, chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. Hali ambayo inatia shaka ni hatma ya ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
“Hatuoni mantiki ya kigugumizi cha serikali ya CCM na viongozi wake, kushindwa kuzungumzia utendekaji wa haki na uwajibikaji kama moja ya misingi muhimu sana ya tunu ya amani.
Masuala haya yakitekelezwa inavyotakiwa, hata kazi ya ulinzi na usalama kwa raia na mali zao, itakuwa rahisi kwa sababu itakuwa ni wajibu wa jamii nzima. Kinyume na hapo, kwa kufumbia macho vitendo vya wazi vya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, ikiwemo isiyoweza kuthaminishwa na kitu chochote, haki ya kuishi, inazidi kujipotezea uhalali wa kutawala.
CHADEMA imeendeleaa kusisitiza kutaka uwajibikaji wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Emmanuel Nchimbi, IGP Saidi Mwema, Kamanda wa Operesheni Maalum wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, RPC wa Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile na RPC wa mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, kutokana na mauaji yaliyotokea mkoani Morogoro na Iringa, kwa wao wenyewe kujiuzulu au kufukuzwa kazi na Rais ili kupisha uchunguzi huru.
“Wakati Kurugenzi ikisisitiza msimamo wa chama wa kuitaka serikali iwakamate na kuwafungulia kesi ya mauaji, Kamanda wa FFU Mkoa wa Morogoro (kwa mauaji ya Ally Zona) na RPC Kamuhanda na askari wote wanaoonekana kwenye picha wakimsulubu marehemu Daudi Mwangosi kabla hajalipuliwa kwa bomu la polisi na kufa, inapenda kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi linawajibu wa kuhakikisha watuhumiwa wa mauaji ya Mbwambo waliotoroka, Samwel Mtinange na Mohamed Limu, wanapatikana huku hatua zinazostahili juu ya tukio hilo la utorokaji zikichukuliwa kwa wahusika wote,” wamesema.
Mbali na waliotoroka, washtakiwa wanaoendelea kushikiliwa kuhusiana na mauaji ya Mbwambo ambaye aliuawa kikatili kwa kukatwa kichwa na kitu chenye ncha kali shingoni kubaki wanne wakiwemo wenyeviti wa serikali za vitongoji wanaotokana na Chama cha Mapinduzi (CCM), Davis Mkumba (Kisambaramajengo) na Mathias Nathan (Magadini) ambapo washtakiwa wengine ni Saidi Florianna Swalihi na Yohana.
Aidha hatua ya Kamanda Sabas kukanusha taarifa kuwa watuhumiwa hao wakati wakitoroka walifanikiwa kumnyang’anya bunduki mmoja wa askari waliokuwa wakilinda, mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakuwa tayari majina yao kutajwa magazetini walilieleza Tanzania Daima kuwa watuhumiwa hao walimnyang’anya silaha aina ya SMG mmoja wa askari polisi aliyekuwa akiwalinda jambo lililozua hofu kubwa miongoni mwa baadhi ya watumishi wa mahakamani ambao baadhi waliamua kujifungia ndani ya vyumba vya mahakama wakihofia mahabusu huyo kuwafyatulia risasi.
Mashuhuda hao waliendelea kudai kuwa mmoja wa mahabusu hao alikuwa wa kwanza kutoka kwenye chumba cha mahabusu na alipomkaribia askari huyo ambaye jina wala cheo chake hakijafahamika alimvamia na kumpora silaha hiyo inayodaiwa kuwa na risasi 30 na kuruka uzio mrefu wa mahakama hiyo.
Jeshi la Polisi limewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kupatikana kwa washtakiwa hao ambapo limetangaza zawadi nono ya shilingi milioni tano kwa wananchi watakaofanikisha kukamatwa ikiwa ni shilingi milioni 2.5 kwa kila mtuhumiwa.
Tanzania Daima

URAIS 2015 : MTEI AMSHUKIA ZITTO


MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amekitikisa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kwa hatua yake ya kutangaza kuwania urais 2015, baada ya mwasisi wake, Edwin Mtei kumuonya kuwa hatua hiyo itasababisha mzozo na mpasuko ndani ya chama.
Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.
Kauli hiyo ya Mtei imekuja siku chache baada ya mbunge huyo kutangaza kwamba hana mpango wa kugombea ubunge mwaka 2015, badala yake anajipanga kuwania urais.
“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga,” alisema Mtei.
Mtei alisema hatua ya mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 umekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.
Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.
Alisisitiza kwamba siyo vibaya kwa Zitto kuonyesha hisia zake, lakini akasema kuwa ndani ya Chadema kwa sasa, kuna watu mbalimbali wanaopenda kuwania urais, lakini hawajatangaza.
“Dk Slaa (Willbrod) anataka, Freeman (Mbowe) anataka, Zitto anataka, hata mimi huenda nikataka kugombea. Hapa hakuna upendeleo, sifa ndizo zitakazoamua,” alisema.
Huku akimwagia sifa mbalimbali Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini, Mtei alisema kwa upande mwingine, Katiba ya Tanzania kwa sasa, inamnyima Zitto sifa za kuwania urais mwaka 2015 kwa kuwa hadi kufikia mwaka huo atakuwa amefikisha miaka 38, huku Katiba ikielekeza kuwa mgombea urais anatakiwa awe na miaka isiyopungua 40.
Alipoulizwa ya kwamba endapo uchaguzi mkuu ujao utafanyika huku Watanzania wakiwa na Katiba Mpya iliyopunguza umri wa kuwania urais, Mtei alisema endapo mbunge huyo atapambana kuhakikisha umri huo unapunguzwa, basi atakuwa ni mbinafsi wa kupindukia.
“Kama yeye akichukua hatua ya kupambana ili Katiba ibadilishwe kwa kuwa anataka kuwania urais, basi itaonekana ni mtu wa ajabu sana; ni mtu mbinafsi na siyo vizuri.”
Zitto apinga
Akizungumzia kauli hiyo ya Mtei, Zitto alisema: “Demokrasia haileti mizozo kwenye vyama vya siasa hata siku moja, bali humaliza mizozo. Udikteta, kuminya fikra huru na mawazo huru, ndivyo huleta mizozo kwenye vyama vya siasa.”
Alisema ni muhimu wazee wakawaacha vijana wawe huru kusema wanachofikiri kwa kuwa uhuru wa fikra na mawazo ni moja ya haki za msingi na moja ya nguzo za demokrasia.
“Namheshimu Mtei kama mmoja wa waasisi na mwenyekiti mwanzilishi wa chama. Chama chetu kimekua na kina uwezo wa kuhimili demokrasia ya ndani,” alisema Zitto akiongeza kuwa miaka 20 tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, nchi inastahili kuimarisha vyama kidemokrasia.
“Ninarudia, nitaomba kupeperusha bendera ya chama changu kwenye uchaguzi wa urais mwaka 2015. Naamini kwamba ninaweza kuwezesha chama chetu kushinda na kuongoza dola na Chadema kutoa rais wakati baadhi ya waasisi wetu wakiwa hai na kuona vijana wao tunavyobadili maisha ya Watanzania na kutimiza ndoto zao,” alisema Zitto.
Alisema ana uwezo, uadilifu na uzalendo wa kutosha kuwa Amiri Jeshi Mkuu na kuunganisha Watanzania kuwa wamoja bila kujali rika, dini wala makabila yao... “Nimejiandaa kisaikolojia kukabili changamoto za ufukara wa nchi yetu.”
Septemba 26, mwaka huu Zitto alitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais mwaka 2015, alipozungumza na wananchi katika mjadala ulioandaliwa na asasi ya kiraia ya Meza ya Duara uliofanyika maeneo ya Soko la Mwanga, mjini Kigoma na kuhudhuriwa na watu zaidi ya 200. Miongoni mwa maswali hayo lilihusu tetesi kwamba anataka kugombea urais katika uchaguzi ujao.
Katika majibu yake Zitto alisema: “Kwanza nataka niwahakikishie watu wa Kigoma msiwe wanyonge… mna uwezo wa kutoa rais wa nchi hii.
“Nimefanya kazi kubwa katika ubunge, nimeleta mabadiliko mengi kuanzia bungeni mpaka jimboni. Nadhani inatosha na hata nikiongezewa miaka mingine sitaweza kufanya yale yaliyonishinda katika kipindi cha miaka 10.
“Kama Mungu ataniweka mpaka mwaka 2015, sitagombea ubunge tena kwa sababu kazi niliyofanya inatosha.Natangaza rasmi kuwa nitagombea urais kupitia chama changu cha Chadema, bila kusababisha msuguano wowote na sitaki kuingia katika historia ya kurudisha nyuma harakati za upinzani kushika dola. 

“Nataka kuleta changamoto mpya, nitawaeleza watu wa chama changu nia hiyo na nitatoa hoja za msingi. Hata kama sitapata ridhaa yao, lakini huo ndiyo msimamo wangu. Iwapo chama kikiona sistahili au sifai, nitakubaliana na uamuzi huo. Watu wengi wanadhani urais ni cheo, hawajui kuwa ni nafasi ambayo inakufanya ufanye vitu ambavyo ni vikubwa na vya maendeleo kwa wananchi.
”
Alipoulizwa kuwa mwaka 2015 atakuwa na miaka 39, hivyo kukosa sifa ya kugombea urais kwa mujibu wa Katiba alijibu: “Nadhani nina uwezo wa kuwa rais, sidhani kama Katiba inaweza kumzuia mtu mwenye uwezo asigombee na ndiyo maana ninaamini kuwa kipengele cha kuwa na miaka 40 kitabadilishwa katika Katiba Mpya.”
Mwananchi

TAMKO LA JOHN MNYIKA KUHUSU WIKI YA VIJANA

TAARIFA KWA UMMA
Tarehe 4 Oktoba 2012 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fennela Mukangara amezungumza na vyombo vya habari kueleza kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Taifa ya Vijana. Waziri ameeleza kuwa maadhimisho hayo yatahusisha maonyesho yatakayoanza tarehe 8 na kufikia kilele chake tarehe 14 Oktoba 2012 kwenye kilele cha mbio za Mwenge na kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere mkoani Shinyanga. Waziri ameeleza kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maonyesho na maadhimisho hayo anatarajiwa kuwa Rais Jakaya Kikwete. WAZIRI AELEZE HATUA ILIYOFIKIWA KATIKA KUANZISHA BARAZA LA VIJANA, BENKI YA VIJANA NA KUPANUA WIGO WA AJIRA KWA VIJANA Nikiwa mmoja wa vijana wa Tanzania na mbunge kijana sikubaliani na utaratibu mzima ulivyopangwa wa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fennela Mukangara kutoa ratiba ya maonyesho na maadhimisho mengine bila kueleza hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwa vijana katika maadhimisho kama hayo mwaka 2011 na pia kuweka mkazo katika maonyesho katika Mkoa mmoja badala ya masuala na matukio muhimu yenye kugusa maisha ya vijana wa katika maeneo mbalimbali nchini mijini na vijijini. Hivyo, natoa mwito kwa vijana katika maeneo mbalimbali nchini kutokubaliana na utaratibu huo wa kuweka kipaumbele katika maonyesho zaidi badala yake wafanye maadhimisho kwa kuweka kipaumbele masuala na matukio yenye kugusa maisha ya vijana na mustakabali wa taifa. Vijana tuitumie wiki hiyo kutafakari masuala ya msingi baina yetu ili tuweze kutimiza wajibu lakini wakati huo huo tuzifuatilie mamlaka zingine zinazohusika na masuala ya vijana kwa upande wao ikiwemo serikali katika ngazi zote kuhusu utekelezaji wa ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa vijana kwa nyakati mbalimbali katika mwaka 2011. Kwa upande wangu, naitaka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ieleze hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa ahadi kipaumbele kuhusu ajira kwa vijana na uundwaji wa Baraza la Taifa la Vijana kama ilivyoniahidi bungeni mwaka 2011 na nyingine kuzirejea bungeni mwaka 2012. Kuhusu masuala ya ajira, tulipendekeza bungeni na Wizara ikakubaliana nasi kuanzisha Benki ya Taifa ya Vijana ili kuwezesha vijana wasioweza kumudu masharti ya kibenki katika mfumo wa kawaida wa kibenki kuweza kupata mitaji kwa masharti nafuu kwa ajili ya kujiajiri. Aidha, tulipendekeza na Wizara ikakubali kushirikiana na Wizara zingine ili kuwe na mfumo wa kuwezesha wahitimu wa vyuo kutumia vyeti vyao kama dhamana kuweza kukopa katika mabenki kwa ajili ya kujiajiri. Kuhusu uundwaji wa Baraza la Taifa la Maendeleo ya Vijana, serikali iliahidi kwamba mchakato wa kuundwa kwa baraza hilo ungekamilika katika mwaka wa fedha 2011/2012, hata hivyo mpaka kipindi hicho kinamalizika mwezi Juni 2012 na kuanza kwa mwaka mwingine wa fedha 2012/2013 ahadi hiyo haijatekelezwa. Baraza la Taifa la Maendeleo ya Vijana likianzishwa litaweza kuwaunganisha vijana bila kujali tofauti zao zingine katika kushughulikia vipaumbele 1 mbalimbali vya vijana ikiwemo katika masuala ya elimu, ajira, afya, michezo na maisha ya vijana kwa ujumla. MAADHIMISHO YA WIKI YA TAIFA YA VIJANA YASIFUNIKWE NA KILELE CHA MBIO ZA MWENGE Oktoba 8 mpaka 14 kila mwaka vijana bila kujali itikadi wanapaswa kuungana kote nchini kuadhimisha wiki ya taifa ya vijana. Hata hivyo, toka wiki hii ilipoanzishwa na Serikali mwaka 2003 imekuwa ikiadhimishwa bila mwitikio wa kiasi cha kutosha katika ngazi mbalimbali isipokuwa katika maeneo ambayo wiki hii imekuwa ikiadhimishwa kitaifa kwa kufanya maonyesho ya namna mbalimbali. Hivyo, nia ya taarifa hii ni kuhimiza vijana, serikali na wadau mbalimbali ili maadhimisho ya mwaka huu yawe na hamasa na maana zaidi kwa maisha ya vijana wa Tanzania na Taifa kwa ujumla. Aidha, maadhimisho ya kila mwaka ya wiki ya vijana yamekuwa yakichanganywa pamoja na kilele cha mbio za Mwenge na Maadhimisho ya siku ya Mwalimu Nyerere kitaifa. Matokeo yake wiki ya vijana imekuwa ikifunikwa na shamrashamra za mbio za Mwenge na hatimaye kupoteza malengo ya msingi ya kushughulikia masuala yanayowagusa vijana moja kwa moja. Pia zaidi ya maadhimisho ambayo yatafanyika kitaifa Shinyanga ni vyema mkazo ukawekwa katika kufanya maadhimisho katika ngazi mbalimbali hususani wilayani. Hivyo maafisa maendeleo wa vijana wa wilaya walau mwaka huu wajitokeze kutembelea vikundi vya vijana,kuratibu matukio ya asasi za vijana na kuhamasisha mijadala ya vijana kuhusu mustakabali wao na taifa kwa ujumla. Taarifa hii inalenga pia kutoa mwito kwa vijana nchini kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya wiki ya taifa ya vijana ya mwaka huu itakayoanza Oktoba 8 ambayo kilele chake kitafikia Oktoba 14. Kila kijana wa Tanzania afanye walau kitu kimoja katika wiki hii kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya jamii-kama ni kusaidia wasiojiweza, kufanya usafi wa mazingira, kufanya majadiliano kuhusu mustakabali wa vijana na taifa, kuonana na viongozi kuzungumza nao kuhusu maendeleo katika maeneo yao kuhusu masuala ya elimu, ajira, afya, ukuzaji wa vipaji vya vijana, michezo, ushiriki wa vijana katika uongozi na mengineyo. Wiki hii ni muhimu kwa sababu kwa upande mmoja, vijana ndio kundi linaloathirika zaidi na mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kijamii yanayojiri nchini kwetu na duniani kwa ujumla. Kwa upande mwingine vijana ndio chachu ya mabadiliko katika taifa lolote duniani kutokana na nguvu, ubunifu, na uwingi wetu
.
Imetolewa tarehe 5 Oktoba 2012 na:
John Mnyika MB
Hivi karibuni Waziri wa Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Terezya Huvisa walitoa tamko kwamba nyumba zote zilizojengwa kando kando ya fukwe za bahari na mito zitabomolewa, bila wamiliki kulipwa fidia kutokana na kukiuka Sheria za Ardhi na Mazingira za mwaka 1992, 1995 na 2004.
Kauli hiyo ilitokana na ukweli kwamba imekuwa ni jambo la kawaida kwa watu wenye nguvu ya fedha kuharibu mazingira kwa makusudi pasipo kujali athari ambazo zinaweza kutokea sasa na baadae kwa wakazi wa maeneo husika, jamii inayowazunguka na taifa kwa ujumla!
Kwa watu wengi, kauli ya mawaziri hao ilionekana kama ni hatua muhimu sana katika kulinda mazingira ya fukwe zetu na jamii nzima hasa kutokana na umuhimu wa kulinda mazingira katika wakati huu wa athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Lakini baadhi yetu tuliona kama ni mwendelezo wa kauli za Serikali ambazo utekelezaji wake ama huwa ni wa mashaka au ukitekelezwa basi utekelezaji wake hutawaliwa na upendeleo wa hali ya juu kwa watu wenye fedha na nafasi kubwa serikalini (vigogo).
 
Moja kati ya nyumba iliyotakiwa kubomolewa imejengwa kwenye viwanja namba 2019-2020 Kawe Beach, katika fukwe za Bahari ya Hindi. Viwanja ambavyo vilipatikana kwa ushirikiano wa Mchungaji Lwakatare na tapeli maarufu wa Ardhi jijini Dar es salaam, anayejulikana kwa jina la Frank Mushi.
Ikumbukwe kwamba katikati ya mwezi Julai, 2012 wananchi waliojenga nyumba katika maeneo yanayosemekana ni tengefu ya Jangwani Beach, Mto Ndumbwi na Mto Mbezi walivunjiwa nyumba katika operesheni iliyoendeshwa na Baraza la Mazingira la Taifa (NEMC).
Operesheni ambayo ilihusisha takriban nyumba 15 na kuta ( fences) 8. Katika nyumba hizo, mojawapo iliyotakiwa kuvunjwa ni ya Mchungaji Getruda Lwakatare.
Lakini kwa sababu ambazo wahusika, akiwemo yeye mwenyewe na serikali, wanazifahamu, nyumba yake haikuguswa! Wakati wananchi wanaofahamu ukweli wa mambo, wakiwa bado wanahoji chinichini juu ya upendeleo wa kitabaka ulio wazi, hivi karibuni wameshuhudia kupitia njia mbalimbali za upashanaji habari, ikiripotiwa kuwa Mchungaji Lwakatare (Mchungaji wa Kanisa la Assemblies of God na Mbunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ) amehamia kwenye nyumba yake mpya. Nyumba ambayo ilipaswa kuwa imebomolewa kwa sababu imejengwa kwenye viwanja ambavyo ni kinyume cha sheria kujenga katika maeneo hayo.
Kuvunja sheria kwa uwazi namna hii, huku wengine wakichukuliwa hatua kwa kuvunja sheria hiyo hiyo, si tu ni ’double standards’, bali kunaweza kutafsiriwa ni kuitia serikali mfukoni. Kitu kibaya zaidi ni kwamba kiongozi huyo alishataarifiwa tangu mapema juu ya ubatili wa kujenga katika eneo hilo, kupitia kwa huyo Frank Mushi kabla hata ujenzi wa nyumba hiyo haujaanza.
 
Ikumbukwe pia kuwa viwanja hivyo vilipatikana na ujenzi huo kuwezekana baada ya eneo la bahari na mto kujazwa kifusi na mawe! Kwa kutambua kuwa kuendelea na ujenzi katika eneo hilo ni kuvunja sheria za nchi zinazohusu utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya jamii nzima, Mchungaji Lwakatare aliendelea kwa kujiificha nyuma ya mgongo wa huyo Mushi, akijifanya hahusiki kabisa na kilichokuwa kikiendelea katika eneo husika. Uthibitisho wa ubatili wa kujenga katika viwanja husika: 1) Tarehe 4/1/2011 Wizara ya Ardhi kupitia barua yenye Kum. Namba LD/297571/18 waliandika barua kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kuhusiana na uvamizi wa kiwanja nana 2019 na 2020 Mbezi Kawe. Barua husika pamoja na mambo mengine ilibainisha kwamba wizara imefanya ukaguzi katika viwanja tajwa, baada ya kupata malalamiko juu ya uharibifu wa mazingira unaoendelea katika eneo hilo. Na kwamba ukaguzi walioufanya umeonesha kuwa ujenzi unaofanyika katika eneo husika hauruhusiwi na unakiuka Tangazo la Serikali (GN) No. 76 ya mwaka 1992.
 
Kupitia barua hiyo, wizara ilimtaka Mkurugenzi wa Halmashauri kuchukua hatua za kubomoa/kuondoa uendelezaji batili uliokuwa ukifanyika katika viwanja Na 2019 na 2020 Mbezi Kawe. Barua hiyo ilisainiwa na Bwana Sadoth K. Kyaruzi, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara. 2) Uthibitisho mwingine ni barua ya tarehe 30/9/2011 kutoka NEMC kwenda kwa Bwana Frank Mushi. Barua husika, ilitoa maelekezo kwa Mushi kuvirudisha katika hali yake ya kawaida, viwanja namba 2019-2020 kwa mujibu wa vifungu 55(2) (a) (e), (3) na 151 (1) ,(2) (a), (b), (3) ,(4) (b) na (f) vya Sheria ya Mazingira, sura 191 ya mwaka 2004.
Barua husika inabainisha kwamba timu ya wataalam toka Baraza la Mazingira (NEMC), Wizara ya Maji, Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam na Manispaa ya Kinondoni ilitembelea eneo husika kufuatia malalamiko kutoka kwa viongozi na wakazi wa Kawe Beach.
Timu hiyo ilibaini kwamba eneo la Mto Ndumbwi, pamoja na bahari lilikuwa linajazwa mawe na vifusi hali iliyosababisha kupatikana kwa viwanja na 2019 na 2020. Ambapo ndani ya viwanja hivyo lilikuwa linajengwa jumba kubwa kinyume kabisa na vifungu 55(2)(a) , 55(2) (b) , 55(2)(d) na 55(2)(e) vya Sheria ya Mazingira. Ilibainika pia kuwa mikoko ilikatwa kinyume na s.63(1) ya Sheria ya Mazingira. Kwa mujibu wa nyaraka nilizonazo, yafuatayo yalijitokeza i) Timu ya wataalam ilibaini kwamba, tayari Wizara ya Maliasili na Utalii ilishatoa zuio la ujenzi katika eneo husika. ii) Manispaa ya Kinondoni, mara kadhaa iliweka zuio la uendelezaji na kutoa amri kwa ’mmiliki’ wa eneo husika kubomoa, lakini mmiliki huyo alipuuza amri hiyo na kuendelea na ujenzi! iii) Ilitolewa amri ya Mahakama, tarehe 5/4/2011 kumtaka Bwana Mushi asiendelee na ujenzi. Amri hiyo ilipuuzwa na ujenzi ukaendelea. Baraza la Mazingira lilimwagiza tena, Bwana Mushi:-2) Kuvunja majengo yote yaliyoko kwenye viwanja vyenye mgogoro. 3) Ndani ya siku saba, tokea amri husika kutolewa (amri ilitolewa 30/9/2011) awe ametoa mawe na vifusi vyote vilivyoharibu mkondo wa maji na bahari na kuurudisha mto na bahari katika hali yake ya kawaida. 4) Ndani ya siku 30 chini ya usimamizi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha kwamba mikoko yote iliyokatwa imerudishwa katika hali iliyokuwa awali. Kwa gharama za Bwana Mushi. Licha ya amri zote hizo, mazuio yote hayo, matamko ya mawaziri yaliyotawaliwa na mbwembwe nyingi, ujenzi uliendelea, nyumba imekamilika. Sasa inatumika.
Wakati kigogo huyo amehamia kwenye nyumba yake kwa matangazo na mbwembwe, Mto Ndumbwi, bahari na mazingira kwa ujumla yameharibiwa vibaya! Bila kusahau kuwa wananchi wengine wamebomolewa nyumba zao kwa kutumia sheria hizo hizo. Kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira, Sura 191 ya mwaka 2004, Fungu 57(1) hairuhusiwi kufanya shughuli zozote za kudumu za kibinadamu ndani ya mita 60 ambazo kwa asili yake zinaweza kuhatarisha au kuathiri vibaya ulinzi na utunzaji wa mazingira, utunzaji wa bahari, kingo za mto, bwawa au mwambao wa asili wa ziwa. Halikadhalika, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 ( Sura 113) Fungu 7 (1) (d) inabainisha kwamba eneo lolote lililo ndani ya mita 60 kutoka kingo ya mto na bahari linatakiwa kutangazwa kama ardhi hatari au kuhifadhiwa.
Na pale inapotokea kuwa masharti ya sheria moja yanapingana na masharti ya Sheria ya Mazingira, kuhusu mambo yanayohusu usimamizi wa mazingira, Sheria ya Mazingira ndiyo hutumika, kwa mujibu wa Fungu 232 la sheria ya mazingira sura Kutokana na hali hii serikali inatakiwa kujinasua katika mwendelezo wa tafsiri wanayoipata wananchi kuwa imetekwa na kuwekwa mfukoni na watu wachache wenye uwezo. Maana wanaona kuwa huu ni mwendelezo wa serikali kuwa na kigugumizi pale sheria zinapovunjwa na vigogo serikalini au watu wenye fedha wanaoshirikiana na baadhi ya viongozi wa serikali na chama tawala kufanya ufisadi. Wameona mambo ya namna hii mara kadhaa, ikiwemo serikali kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kashfa kubwa za ufisadi kama ’akina’ Kagoda na wenzake (EPA), Richmond na kashfa nyingine nyingi. Kwamba sasa inazidi kuonekana dhahiri kuwa kuna watu wako juu ya sheria za nchi, huku wanyonge wakishughulikiwa.
Ni wakati mwafaka sasa kwa mawaziri wanaohusika na masuala ya ardhi na mazingira kuwaeleza Watanzania kulikoni wananchi wa hali ya chini kuvunjiwa nyumba zao kwa kigezo cha kuvunja sheria wakati huo huo Mchungaji Lwakatare (kigogo) ambaye uharibifu wake ni wa hatari kuliko hata hao waliovunjiwa akitamba mtaani kwamba yeye yuko juu ya sheria na hakuna mamlaka yoyote yenye uwezo wa kumzuia kufanya alichofanya! Ni aibu kwa Taifa kuwa na viongozi wa aina hii! Viongozi ambao wako tayari kutumia fedha, hila, mamlaka na dhamana za uongozi walizopewa, kuhalalisha haramu, ni janga kwa mstakabali wa taifa letu!
 
Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi ,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Imetolewa Dar es Salaam na;
Halima Mdee (MB)

Waziri Kivuli, Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi

Picha za M4C Terrat Simanjiro

Kamanda Lema akitoa kadi kwa wananchi


Jackson Makala na James Olle Millya




Friday 5 October 2012

DAR NI SISI- BAADHI YA WANANCHI WAKIELEZEA HALI HALISI YA MAISHA YA DAR



VIDEO BY TWAWEZA ORG.

Sumaye ateta na Chadema


NI KUHUSU MUSTAKABALI WAKE KISIASA

SIKU chache baada ya kushindwa katika uchaguzi wa ndani kwenye nafasi ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amekutana na viongozi wa Chadema ikidaiwa kuwa ni kujadili pamoja na mengine, uwezekano wa kuhamia huko ili agombee urais katika Uchaguzi Mkuu ujao 2015.

 
Sumaye ambaye anatajwa kuwa alikuwa na mpango wa kuwania urais kupitia CCM, alishindwa katika uchaguzi wa kuwania ujumbe wa Nec, baada ya kupata kura 481 dhidi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu aliyepata kura 648.
 
Taarifa zilizothibitishwa na baadhi ya viongozi wa Chadema, zimeeleza kuwa Sumaye hakuridhishwa na mchakato wa uchaguzi huo wa Nec na kwa matokeo hayo, alikutana na viongozi wa Chadema kujadili mustakabali wake kisiasa.
 
Jana, mjumbe mmoja wa Kamati Kuu ya Chadema, ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, alithibitisha Sumaye kukutana na viongozi wa Chadema. Hata hivyo alisema hawajafikia mwafaka.
 
Alisema mawasiliano ya Chadema na Sumaye yalianza mara tu baada ya matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika Septemba 30, mwaka huu yaliyomwengua kigogo huyo kwenye kinyang’anyiro hicho.
 
“Ni kweli kuna watu wa CCM tumewasiliana nao baada ya uchaguzi ule (wa Nec) na Sumaye tunawasiliana naye pia lakini siwezi kusema tumefikia wapi,” alisema mjumbe huyo na kuendelea: “Suala kwamba amekubaliwa kujiunga na Chadema au la, nadhani huu ni uamuzi wake. Ninachoweza kusema ni kwamba vikao vilikuwepo na vinaendelea kukaliwa.”
Alisema baada ya matokeo ya Hanang’ na hali ya kisiasa ndani ya CCM, Chadema kimekuwa kikiwasiliana na Sumaye na kikubwa ambacho kinajionyesha ni kada huyo wa CCM kutoridhishwa na hali ya mambo ndani ya chama chake.
 
Mjumbe huyo wa Chadema alisema chama hicho Wilaya ya Hanang’ kinaandaa mkutano maalumu wa kuwapokea wanachama wapya wa CCM, wengi wao wakiwa baadhi ya walioanguka kwenye uchaguzi wa Nec wilayani humo.

Habari zaidi zimeeleza kuwa Chadema kimepanga siku yoyote juma lijalo, kuwapokea wanachama wapya kutoka CCM, baadhi wakiwa wale walioshindwa kwenye uchaguzi wa ndani ya chama hicho uliofanyika wilayani Hanang’.

Mmoja wa watu wa karibu na Sumaye alisema anachojua ni kwamba Chadema wanamtaka Sumaye na siyo Sumaye kukitaka chama hicho cha upinzani.

“Wamekuwa wakimfuatafuata mara nyingi na mazungumzo ya aina hiyo si mageni baina ya Sumaye na Chadema. Ila ninachoweza kusema, safari hii chochote kinaweza kutokea kutokana na hasira alizonazo (Sumaye). Ngoja tusubiri, atafanya mkutano na waandishi Jumapili.”

Sumaye, Mbowe wazungumza
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Sumaye alisisitiza kuwa atazungumzia masuala yote yanayohusiana na uchaguzi huo wa Hanang’ atakapokutana na waandishi wa habari, Dar es Salaam.

 
“Nitakutana na waandishi wa habari kuzungumzia kilichotokea naomba tu mwendelee kunipa muda,” alisema Sumaye na kuongeza kuwa alikuwa akijiandaa kwa safari ya kwenda Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema asingependa kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yeye si msemaji wa Sumaye... “Sitaki kumzungumzia Sumaye. Mimi si msemaji wake. Tumsubiri yeye azungumze kuhusu hilo.”
Kada wa CCM Hanang’ anena

Katika hatua nyingine, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Hanang’, Goma Gwaltu amekionya chama hicho kuwa kisipodhibiti vitendo vya rushwa katika chaguzi zake, kitakufa.
Gwaltu alisema jana kwamba kwa mazingira yaliyopo sasa ndani ya CCM bila hatua kali kuchukuliwa, kiongozi asiye na fedha hawezi kushika uongozi na ndiyo sababu anaungana na wana-CCM wengine katika wilaya hiyo, ambao wanafikiria kukihama chama hicho.
 
“Kama wewe una nia ya kuendelea na siasa siyo rahisi kushinda hapa Hanang’ ukiwa hukubaliani na watu fulani, sasa mimi naona ni bora tu kutafuta chama kingine kwani siyo dhambi,” alisema Gwaltu bila kuwataja ambao wanataka kuhama CCM.
 
Hata hivyo, Gwaltu alisema kwa upande wake, hafikirii kuendelea na mambo ya siasa wala kulalamika makao makuu ya CCM kuhusiana na alichokiita hujuma alizofanyiwa

Kwa habari kamili tembelea:
 

MBUNGE WA MUSOMA MJINI, VICENT NYERERE (CHADEMA) AMETOA RUNIGA KWA WAFANYABIASHARA WA SOKO KUU LA MUSOMA ILI WAWEZE KUPATA HABARI WAWAPO KAZINI

MBUNGE wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere (CHADEMA), amekabidhi runinga 10 kwa wafanyabiashara wa soko kuu la Musoma mkoani Mara. Mbunge huyo alikabidhi runinga hizo jana, zenye thamani ya Sh milioni 9, katika eneo la ndani ya soko hilo lenye wafanyabiashara wengi.

Nyerere alisema kuwa, wafanyabiashara wa sokoni wamekuwa wakikosa haki ya kupata habari za uhakika, kutokana na kushinda kutwa nzima sokoni.

“Wafanyabiashara wa sokoni ni watu wa kuhangaika, hawana televisheni katika maeneo yao ya kazi na wanaporudi nyumbani, hupata habari za kusikia kwa watu,” alisema.

Amesema runinga hizo zitawasaidia kupata habari za mambo mbalimbali yanayoendelea nchini, ikiwa ni pamoja na uendeshwaji wa vikao vya Bunge.

“Wanapitwa na mambo mengi, vikao vya Bunge huanza asubuhi muda ambao wafanyabiashara hawa wapo sokoni, wanakosa haki ya kupata habari,” alisema.

Akipokea runinga hizo kwa niaba ya wafanyabiashara, Ofisa Biashara wa Manispaa ya Musoma, God Machumu, alimpongeza mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake kwa wananchi.

Mbali ya kupokea runinga hizo, wafanyabiashara hao walimweleza mbunge huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika soko hilo.

Miongoni mwa changamoto hizo, ni pamoja na usumbufu nyakati za masika, kutokana na soko hilo kujaa maji, hali inayosababishwa na soko hilo kukosa mitaro ya maji.

Tatizo la ulinzi katika soko hilo limeelezwa kuwa, kikwazo katika maendeleo ya wafanyabiashara hao kwa madai kuwa, wamekuwa wakiibiwa mali zao kutokana na kutokuwepo kwa ulinzi wa kuaminika.

Thursday 4 October 2012

Dr Slaa kutikisa Arusha Siku ya Jumamosi

 
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anatarajiwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika jiji la Arusha siku ya Jumamosi tarehe 06.10.2012 kuanzia saa 8 mchana. Pamoja na mambo mengine Kiongozi huyo wa CDM pia atatumia mkutano huo kuzindua rasmi kampeni za udiwani katika kata ya daraja mbili,uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vilivyopo mtaa wa NDARVOI.

Tayari kuna hekaheka kubwa katika jiji la Arusha kuhusiana na mkutano huo ambapo mazungumzo ya watu mbalimbali yanazungumzia mkutano huo unaotarajiwa kuwa gumzo.

Taarifa za awali zinasema mkutano huo pia utatumika kufuta nyayo za chama cha CUF ambacho kilisomba watu Dar-es-Salaam kwenda kuwahutubia Arusha ili kuepuka aibu ya kukosa watu.Pia inadaiwa wananchi wa Arusha wamedhamiria kuonyesha dunia uungaji mkono wao kwa chama cha CDM.

Zitto Kabwe Achangia Bima Ya Afya Ya Mjane Wa Mwangosi Na Wanae Kupitia NSSF

KATIKA siku ya mwisho ya harambee ya kumchangia mjane wa marehemu Daud Mwangosi, Ndugu Zitto Kabwe amejitolea kumchangia mjane wa marehemu kwa kumlipia ada ya uanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Kijamii (NSSF) kwa kila mwezi na kwa miaka mitatu mfululizo.

" Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, mimi naona ni muhimu pia mjane akawa na hakika ya huduma ya afya yake na watoto wake wanne. Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya na kwa miaka mitatu." Anasema Zitto Kabwe alipoongea na Mjengwablog.com, mtandao wa Kijamii ulioratibu harambee ya mjane wa Daud Mwangosi.

Hii ni mara ya pili kwa Ndugu Zitto Kabwe kuchangia kwenye masuala ya kijamii kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com, mara ya kwanza ni alitoa mchango wake pale Mtandao wa Mjengwablog.com ulipoendesha harambee ya kuwachangia watoto wa Somalia waliokuwa katika hatari ya kufa kwa njaa. Katika harambee iliyomalizika Jumapili ya Septemba 30 mwaka huu na iliyochukua kipindi cha mwezi mmoja,zaidi ya shilingi milioni tano na nusu zimekusanywa.

Mchango huo wa Ndugu Zitto Kabwe una maana mjane wa marehemu ataweza kuwa na hakika ya yeye na watoto wake wanne kupata huduma za afya bila kufikiria malipo kwa kipindi cha miaka mitatu. Baada ya hapo,michango ya mjane huyo ya kila mwezi kwa mfuko huo wa hifadhi ya kijamii ( NSSF) ambayo atakuwa akilipiwa na Ndugu Zitto Kabwe itakuwa ni malimbikizo ya akiba yake ambayo mjane atakuwa na uwezo wa kuichukua kama akipenda. Kwa sasa mjane wa Daud Mwangosi hayuko kwenye utaratibu wowote wa Bima ya Afya, kwake yeye na wanawe.

Harambee ya mjane wa Daud Mwangosi iliyoendeshwa kwa uwazi kwa njia ya MPESA, TigoPesa, Airtel Money, NMB Mobile na Western Union ilimwezesha mchangiaji kuliona jina lake na mchango wake kwenye orodha ya wachangiaji iliyokuwa ikiwekwa mtandaoni kila siku.

Michango ilikuwa ni hiyari, hakuna aliyeombwa kutoa na utaratibu haukuruhusu ahadi za kuchangia, bali, mwenye nacho alitoa na hapo hapo kuorodheshwa kama mchangiaji. Utaratibu haukuruhusu pia michango iliyofungamana na siasa za vyama.

Hatua hiyo ya uwazi na kutanguliza ubinadamu na si itikadi kwenye uchangiaji imechangia kupelekea Watanzania wengi wa kada zote, kwa namna moja au nyingine kushiriki kwenye kuchangia. Kuna waliochangia shilingi elfu moja na kuna waliochangia mpaka shilingi milioni moja.

Ari hii ya Watanzania kujitolea kusaidiana kwenye hali kama iliyomkuta mjane wa Daud Mwangosi imedhihirisha umoja na upendo tulionao kama Watanzania, na pia imeonyesha jinsi tunavyoijali amani yetu na hivyo jamii, kupitia michango hii, imeonyesha pia kwa vitendo, dhamira ya kulaani kwao vitendo vya maovu na vinavyotokana na matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima kama kile kilichomtokea mwandishi Daud Mwangosi.

Baadhi ya watu maarufu katika jamii waliojitokeza kwa hiyari yao kumchangia mjane wa Daud Mwangosi kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy- Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku ( Mmiliki wa Fullshangwe.blog) na Ndugu Mobhare Matinyi aliyepata kuwa mhariri wa gazeti la Majira.

Michango kwa mjane wa Daud Mwangosi itaingizwa kwenye akaunti ya mjane ya CRDB, Iringa leo alhamisi, Oktoba 4, 2012. Vielelezo vya kibenki vitawekwa kwenye mtandao wa Mjengwablog.com kwa kila mmoja kuona jumla iliyowasilishwa kwa mjane na orodha ya majina ya wachangiaji.

Chanzo: http://www.mjengwablog.com/2012/10/zitto-kabwe-achangia-afya-ya-mjane-wa.html
MIAKA michache iliyopita niliandika makala ndefu sana nikiwashauri Watanzania wenzangu waliokuwa wanapigania sana vyama viungane ili kuwa na upinzani dhidi ya chama tawala na hatimaye kukiangusha chama tawala.
Naomba nikupitishe kwa kifupi sana msomaji wa kona hii kwenye makala ile ya Oktoba 8, 2008.

Niliamua kutumia makala nzima kueleza kwa kinagaubaga mawazo yangu kuhusu ushirikiano wa vyama vya upinzani ambao ulikuwa ukipigiwa upatu sana na Watanzania kwa muda mrefu. Siku hiyo niliwaambia kwamba ni vema ushirikiano wa vyama vinne vya upinzani (CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na TLP) ukavunjika kwa masilahi ya taifa.


Nilieleza jinsi vyama vya upinzani vilivyoungana Kenya lakini baada ya kuing’oa KANU kulizuka mgogoro wa chama hiki kudai kupewa mawaziri wachache, kile kikidai kunyimwa wizara nyeti, hiki hapa kikidai makubaliano yamekiukwa na mambo kadha wa kadha mpaka wakagombana. Walisambaratika na kumlazimisha Rais aliyetokana na upinzani kuanzisha ushirikiano mpya na Rais aliyeondoka madarakani na hivyo kufifisha vita dhidi ya ufisadi na kusababisha serikali iliyokuwa madarakani ionekane ya ufisadi sawa na ile serikali iliyokuwa imepita.


Huo ndiyo ushirikiano wa vyama vya upinzani unaotafutwa na Watanzania?


Niliwatahadharisha Watanzania kwamba hatuhitaji ushirikiano wa vyama vya upinzani wenye lengo la kuing’oa CCM madarakani. Tunahitaji Tanzania mpya yenye kutoa fursa kwa kila raia kufaidi rasilimali za nchi hii na kujiletea maendeleo bila kujali katokea kundi gani.


Ushirikiano wa CHADEMA, CUF, NCCR na TLP hautafanikisha hayo.


Niliwashauri Watanzania tuwaruhusu wapinzani wavunje ushirikiano wao halafu wajijenge kama chama kimoja kimoja na ndipo tutakapoona chama chenye mwelekeo wa kuleta maendeleo tukipe kura.


Siku hiyo nilisema: “Natamani chama kama CHADEMA, ambacho kimejipambanua hivi karibuni kuwa chama makini chenye sera nzuri zilizopata kusifiwa hata na Mwalimu Nyerere wakati wa uhai wake na ambacho hivi karibuni kimewaonyesha Watanzania kwamba kumbe inawezekana kuiondoa CCM na tukaongozwa na chama kingine na kujipatia maendeleo ambayo hatukuwahi kuyaota wakati wote wa CCM, kipate kukubalika toka kwa Watanzania.


Wakipokee na kukipa nafasi ya kujipanua na mwaka 2010 kuwe na uchaguzi wenye ushindani kama tuliokuwa tunaushuhudia Tarime.


Vyama vingine viendelee kusimamisha wagombea urais, ubunge na udiwani kwa kuwa ni haki yao lakini mchuano uwe kati ya vyama viwili kama tulivyoona kule Tarime na hapo ndipo tutakuwa tunaelekea huko kwenye maendeleo.


Hayo yalikuwa baadhi tu ya maneno niliyoyasema wakati huo. Ni kama CHADEMA waliisoma makala ile kwa makini na kuielewa kwa kuwa muda mfupi baadaye walitangaza kuvunja ndoa ya upinzani na kuanza kujiimarisha kama chama peke yake chenye malengo ya kuchukua dola kwa kutumia sera zake chenyewe na kuepuka mtego wa kuungana na baadaye kuanza kupigana ni sera za chama gani kwenye ushirikiano zitekelezwe.


Wakaanzisha kile kilichojulikana kama Operesheni Sangara ambayo kwa kiwango kikubwa ilikidhoofisha sana chama tawala sanjali na vyama vingine vya upinzani.


Watanzania wakaanza kuielewa CHADEMA kama chama. Februari 11, 2009 nikaandika makala nyingine yenye kichwa cha habari, “CHADEMA na CUF wanahitaji msaada wako.”


Katika makala ile nikaomba kura ya maoni ikiwa vyama hivyo viwili viungane ama viendelee kujijenga kila kimoja kivyake! Wengi wakasema kila chama kijijenge kivyake, sababu zilikuwa nyingi na zote niliziandika katika makala iliyofuata.


Operesheni Sangara ilikuwa kama mashambulizi ya anga vitani. Mashambulizi ambayo siyo siri kwamba yamevidhoofisha mno vyama vikubwa kama CCM na CUF.


Ushahidi wa hili ni matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ambapo CHADEMA ilipaa kutoka majimbo mtano ya ubunge iliyoyapata 2005 mpaka 23 mwaka 2010.


Wabunge viti maalumu kutoka 6 mpaka 25. Halmashauri za wilaya zinazoongozwa na CHADEMA kutoka vitatu mpaka saba.

Kura za urais kutoka laki sita mpaka mpaka milioni 2 na ushee, madiwani idadi ikaongezeka zaidi ya mara tano.
Kuimarika huku kwa CHADEMA hakuwezi kutokea bila kuviathiri baadhi ya vyama.


CCM kwa mfano majimbo yote ya CHADEMA yaliyoongezeka yalitoka mikononi mwa CCM, halmashauri zote zilizoongezeka kuongozwa na CHADEMA zilitoka mikononi mwa CCM, kura za urais zilipoongezeka zilipungua za CCM na CUF, kambi rasmi ya upinzani bungeni sasa ikapokwa mikononi mwa CUF ambayo imeiongoza kambi hiyo tokea mwaka 1995 na uongozi wa kambi sasa ukachukuliwa na CHADEMA.


Ruzuku ya CCM sanjali na ya CUF zinapungua wakati ya CHADEMA ikiongezeka kutoka milioni 60 kwa mwezi hadi milioni 230 kwa mwezi. Watanzania wakazidi kuipenda CHADEMA na wito wangu katika makala ile wa kuwataka Watanzania wakikumbatie hiki chama kama chao na kukiimarisha tayari kwa kukifanya chama mbadala wa kilichoko madarakani ukaonyesha kupokelewa na kutekelezwa barabara.

Safari ya CHADEMA kuelekea Ikulu ikaanza rasmi.


Ulipotokea uchaguzi mdogo Arumeru Magharibi, CHADEMA iliingia kwenye uchaguzi huo na kumbukumbu ya kipigo (hata kama kilikuwa cha haramu kama ilivyothibitishwa na mahakama hivi karibuni). Nikiwa mmoja wa viongozi wa chama tena nikiwa ndiye mwenyekiti wa mkoa wa Arusha ambamo ndimo kulikuwa na uchaguzi huo mdogo wa Arumeru, ilibidi kukaa na kufanya maamuzi.


Jambo la kwanza tulinuia hakuna kushindwa Arumeru kwa kuwa mtanange ilikuwa umekuja nyumbani ingelikuwa ni aibu kushindwa tena hata kama ushindi wa CCM ungelikuwa wa magumashi kama ambavyo imefanya siku zote.


Tukamuacha katibu mkuu wa chama akiwa na makamanda wengine katika kuhakikisha kampeni zinaanza na mikakati mingine ya kawaida ya kampeni zetu inaendelea.


Uongozi wa mkoa ukaungana na Mwenyekiti Taifa, Mkurugenzi wa Raslimali Taifa na Mkurugenzi wa Fedha Taifa, tukakaa pamoja kuandaa mkakati wa pekee wa ushindi ikiwa ni pamoja na kupata fedha na raslimali zingine kwa ajili kuendesha kampeni.


Ni katika kukaa wakati huo ndipo tulipokuja na wazo la M4C ama “Movement for Change” ama “Vuguvugu la Mabadiliko” kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili. M4C ikanuia kukikabidhi chama kwa wananchi. Wazo lilelile nililolizungumza kwenye makala yangu mwaka 2008.


Wanachama wakaipokea M4C nchi nzima. Wakachanga pesa na rasilimali nyingine na kiukweli kilichonishangaza zaidi ni kitendo cha wana CCM wengi wa chini kuipokea M4C na kuipa sapoti kubwa.


Katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki wana CCM walifanya kazi ya ziada kuibeba CHADEMA. Walitupatia kura zao na za ndugu zao lakini zaidi walifichua hujuma nyingi sana zilizokuwa zinaandaliwa na CCM juu yetu. Tukapata ushindi wa kishindo!

Tukaikabidhi M4C kwa chama taifa na likawa sasa ni vuguvugu la nchi nzima. Kamati Kuu ikaamua kwa makusudi kuiboresha M4C ili itembee kwa mpangilio nchi nzima. Wakaamua kwamba sasa M4C ya kitaifa izinduliwe Dar es Salaam ili kufuta propaganda ya kwamba CHADEMA ni chama cha kaskazini tu.
Kutoka kwenye uzinduzi Dar es Salaam kwa makusudi kamati kuu ilikuwa imeelekeza M4C ielekee Mtwara na Lindi, eneo la ukanda wa Pwani ya kusini ambako CCM imekuwa ikidanganya watu kwamba CHADEMA haiwezi kwenda kwa sababu ni eneo la Waislam wengi na CHADEMA ni chama cha Wakristo.


Kazi iliyofanywa huko na M4C ya CHADEMA wanaoweza kusimulia vizuri ni kina Bernard Membe, George Mkuchika, Mathias Chikawe, Hawa Ghasia na wenzao ambao walikimbia majimboni kwenda kushuhudia. Kule CHADEMA ilifuta utawala wa CUF na CCM uliodumu miaka mingi.


Ili usipate shida ya kuniamini mimi au wale wasioitakiwa mema CHADEMA, ni vizuri ukaenda mwenyewe kufuatilia na kujua CHADEMA inaendeleaje huko kwa sasa.


M4C inafanyaje kazi. Imegawanywa katika vikosi vinne na awamu nne tofauti.


Kwanza hutangulia kikosi cha tathmini kinachokwenda kukagua hali ya chama na uongozi wa wake.


Hiki huweza kuja na majibu yanayoonyesha chama kiko katika hali gani na ni maeneo gani yanahitaji kuongezewa uzito.


Baada ya ripoti yao huja kikosi cha hamasa ambacho hufanya mashambulizi ya anga kwa njia ya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kuhamasisha na kuingiza wanachama wapya.


Baadaye huja kikosi cha tatu ambacho kazi yake ni kusimamia uchaguzi tangu ngazi ya matawi mpaka kata.


Na mwisho huja kikosi cha mwisho ambacho hutoa mafunzo kwa viongozi waliochaguliwa kuwafanya wakijue chama waijue katiba ya chama, kanuni za uendeshaji chama, taratibu na maadili ya viongozi na wanachama ili waweze kuongoza vizuri chama kwa mujibu wa katiba, kanuni na maadili chama. Na vikosi hivyo vinapoondoka, vinaacha viongozi wa matawi na kata wakishuka kuweka kusimika viongozi wa misingi na mabalozi wa nyumba kumi wa CHADEMA. Wapi CCM itaponea? Wapi CUF itatokea? Hapo ndipo CCM ilipokiona kifo chake na CUF ikaanza kunusa kuzidi kudumaa kwake.


Unapomsikia leo Mwenyekiti wa CCM taifa anajiwahi wahi kusema CCM haifi kabla hajaulizwa, ni kile kile alichokisema Ansbert Ngurumo Jumapili iliyopita kwamba ni kama mlevi ambaye amelewa chakali na anatembea barabarani kwa kuyumba yumba na kuanguka hovyo, anapopishana na watu anaona wakimshangaa anaanza kupaza sauti: “Nani kasema mimi nimelewa? Sijalewa mimi!”


Kikwete kasoma nyuso za Watanzania na alipofika ukumbini akasoma nyuso za wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama chake, kama mlevi akaona wajumbe wakishangaa jinsi alivyochoka na chama kinamfia mikononi mwake. Kama yule mlevi akaanza kupaza sauti: “Kina nani wanasema CCM inakufa? CCM haifi bali wanaoiombea kifo watakufa wao na kuiacha imara!”


Naam, kupitia M4C CCM inakiona kifo chake kinavyokuja kwa hakika tena chafanya haraka. CUF nao wanaziona dalili za kunyauka kwani watabaki na mzizi mmoja tu ule wa Pemba ambao kwa kibaiolojia hauwezi kupitisha maji na madini ya chumvichumvi ya kuulisha mti mkubwa wa nchi nzima uitwao Chama cha Wananchi (CUF).


Ndiyo maana M4C ilipohamia Morogoro, Iringa, Dodoma, Singida na Manyara, ilibidi CCM na serikali yake watumie nguvu za dola kuizima na kuifanya isiendelee ili wenyewe wabaki madarakani.


Lakini niliwahi kusema huko nyuma baadhi ya watu wakanishambulia. Kwamba CHADEMA kina mkono wa Mungu maana hata yeye amechoka kuona watanzania wakiteseka hivi, ameleta mkombozi. Mbinu ya kutumia dola imeshindwa baada ya kifo cha Mwangosi. Sasa wamebuni kitu kipya. CCM wanaungana na CUF kuikabili M4C ya CHADEMA.


Ni bahati mbaya kwamba katika mkakati wao wameamua kuanzia Arusha. Walidhani kwa kuwa Arusha ni ngome ya CHADEMA na vijana wa Arusha hawana mchezo linapokuja suala la kutetea chama chao, wakadhani watawachokoza halafu CHADEMA watajibu kwa kuwafanyia vurugu na kisha serikali ya CCM iseme, “Mikutano ya kisiasa kwa sasa imekuwa chanzo cha uvunjivu wa amani.


“Kwa hiyo serikali imesitisha mikutano ya vyama vyote mpaka hapo hali itakapotulia.”


Itatulia lini, anajua waziri wa mambo ya ndani na jeshi lake la polisi na usalama wa taifa. Kwa kufanya hivyo watakuwa wamezuia M4C isiendelee. Ndugu yangu Mtatiro, wewe ni rafiki yangu sana. Nimeandika makala kadhaa kukutetea ulipokuwa unashughulikiwa pale Mlimani kwa sababu za kisiasa. Lakini katika hili sitakubaliana nawe niko tayari uniseme utakavyosema.


Ili kuonyesha kwamba ni mkakati, Mtatiro ulikuwa Dar es Salaam wakati ‘advance team’ yenu ilipokuja Arusha kuhamasisha ujio wa Ibrahim Lipumba, mheshimiwa mwenyekiti wenu taifa. Walifanya mikutano michache, mimi nilishuhudia mmoja tu pale Mbauda Sokoni ambapo walihutubia mkutano uliohudhuriwa na wananchi 11. Walikuwa wakihutubia kwa amani tele. Shida ilikuja pale walipokuta wamachinga wakiwa katika harakati za kujitwalia kwa nguvu kiwanja cha wazi kilichouzwa kifisadi kwa mtu binafsi.


Uuzaji ambao ulisababisha meya wa Arusha wakati huo ajiuzulu. Walikuwa wameziba barabara iendayo Kilombero sokoni. Gari la matangazo la CUF likaja.


Wakawaomba wageuze na kutumia barabara nyingine. Hawakutaka wakawa wanalazimisha kupita pale wakiimba nyimbo za CUF na kuwaonyesha ishara za chama chao.


Wamachinga wachache wakaamua kuwaonyesha alama ya CHADEMA pengine kuwaonyesha kwamba sisi wengine ni wanachama wa CHADEMA kwa hiyo hatuna haja ya kuonyeshwa alama za CUF.


Mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari la matangazo la CUF akaamua kuwaonyesha wamachinga wale alama ya vidole vya kuonyesha matusi. Hapo ndipo wamachinga walipokasirika na kuwarushia mawe. Kumbe ni mtego uliopangwa, saa hiyo hiyo Mtatiro akarusha kwenye mitandao kwamba Wanachadema wamewashambulia wana CUF.


Baadaye wameleta Coaster zaidi ya nane kuja kuhudhuria mkutano wao wa Lipumba. Wakiwa njiani huko walipoulizwa na watu ambao hawakujua kama ni CHADEMA wakawa wanasema wanakwenda Arusha kulipiza kisasi cha watu wao kupigwa na CHADEMA. Wamekuja, Lipumba kahutubia hao watu wake aliowatoa Dar es Salaam na wana Arusha wasiozidi 100.


Kahutubia kwa amani kaondoka na hakuna badiliko lolote! Magazeti ya kesho yake hayakupata hata kuiweka habari yao ukurasa wa mbele isipokuwa yale ya wabia wao CCM ambayo yalidiriki kusema eti diwani wa CHADEMA ahamia CUF wakati wakijua huyo mtu alifukuzwa uanachama na CHADEMA na kupoteza hata udiwani. Anakuwaje diwani wa CHADEMA? Kwa hiyo V4C ilijifia kabla hata haijaanza kama walivyotabiri waandishi wenzangu.


Na mkakati wa pamoja kati ya CCM na CUF nao umefeli kabla ya majaribio jijini Arusha. Labda niwashauri wakaanzie huo mkakati Pemba
 

Chadema UK Ndani ya Milton Keynes

DAR NI SISI - VIDEO MAISHA YA WANADAR HATA BAADA YA MIAKA50 YA UHURU