Jiunge na harakati
Wanachama ndio kiini cha chama chetu. Kama utajiunga nasi leo utakuwa ni sehemu ya harakati za kampeni ya mabadiliko. Harakati zenye lengo la kuleta mabadiliko ya kweli katika nchi yetu ya Tanzania.
kama mwanachama utakuwa na uwezo, haki na uhuru wa kuchangia sera mbalimbali za chama, kushiriki na kufanikisha mipango, shughuli na kampeni mbalimbali za chama, uwezo na haki ya kuchagua viongozi wa chama, kuchaguliwa kuongoza na kuwakilisha katika ngazi mbalimbali za chama pamoja na kushiriki katika vikao mbalimbali vya chama.
Ili kuwa mwanachama na kujiunga katika harakati za mabadiliko tafadhari download na jaza fomu ya uanachama kisha tutumie kwa barua pepe au Posta.
Email: chademauk@gmail.com
No comments:
Post a Comment