Tawi la Chedema UK limekusudia kukusanya £ 20,000/- kufikia Mwezi Disemba Mwaka 2012, fedha kwa ajili ya kusaidia kampeni ya M4C na kuchangia huduma za afya Tanzania. Tunakusudia kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya uhamasishaji wa kampeni kama vile Baiskeli, Pikipiki pamoja na magari ya bei nafuu ili kuwafikia watu wengi zaidi hususani wananchi waliopo vijijini. Pia tumedhamilia kuchangia huduma za afya nchini kwa kununua vifaa mbalimbali vya huduma ya afya ili kuboresha utoaji wa huduma za afya mahospitalini.
Ili kufikia malengo yetu tunawaomba Wanachama, Watanzania na Wadau mbalimbali wanaopenda mabadiliko na maendeleo ya nchi yetu kuchangia na kushirika katika harakati hizi za mabadiliko ya kweli.
Pia unaweza kushiriki kwa kuandaa fundraising mbali mbali kama vile Matembezi, mbio, Chakula, Pati, Matamasha ya Muziki na Burudani n.k
Kwa maelezo zaidi na Kuchagia tutumie barua pepe kupitia chademauk@gmail.com
No comments:
Post a Comment