MBUNGE wa Arumeru Mashariki,
mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw.
Joshua Nassari, ameshikilia msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika
jimboni kwake na kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa maendeleo
yao.
Aliwataka wananchi jimboni
humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa mashamba makubwa
yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe wavumilivu.
Bw. Nassari aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara uliofanyika
kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.
Aliwaataka wananchi kuupuuza
mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na kusisitiza kama mtu yeyote
atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge amualifu.
“Sioni sababu ya Mwenge wa
Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani badala ya kuhamasisha maendeleo,
umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za wananchi.
“Hali hii inachangia umaskini
wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo yote ambayo mwengu huu unalala,
nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku kufika jimboni kwangu.
“Mtu yeyote ambaye ataombwa
mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima
baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema Bw. Nassari.
Aliwataka wananchi hao
kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao kisiasa na
kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia maadili ya utendaji kazi na kuacha
kuwabughudhi wananchi kwa kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru
sokoni kupitia wakala wao.
Akizungumzia suala la uvamizi
wa mashamba, Bw. Nassari
aliwataka wananchi kuwa
wapole kwani anaandaa mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka mitatu, wamiliki wa
mashamba hayo wanakimbia wenyewe ili wananchi waweze kujitwalia ardhi
yao.
Katika hatua nyingine, Bw.
Nassari alisema fedha zilizotengwa na halmashauri kwa maendeleo Kata ya Usa
River, kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi June mwaka 2013, ni sh. milioni 54.3
ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na huduma ya maji safi.
Alisema ukarabati wa barabara
kutoka Usa River hadi Magadilishu umetengewa sh. milioni nane na barabara za mji
mdogo katika kata hiyo zenye urefu wa kilometa tano, zitagharimu sh. milioni
75.
Katika mkutano huo, wafuasi
15 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Tanzania Labour Party (TLP) walitangaza
kuvihama vyao vyao na kujiunga CHADEMA.
Majira
Monday, 17 September 2012
Sunday, 16 September 2012
TASWIRA MBALI MBALI ZA MKUTANO WA CHADEMA MILTON KEYNES
Engineer Prudence akishusha madongo mazito.
|
Mchungaji Mathew akimwaga sera. |
Dr John Lusingu akitoa mifano hai |
Mwenyekiti wa Chadema-UK Chris Lukosi akihutubia |
Kamanda Makelele, Katibu mwenezi wa moshi mjini aki wapa nasaha viongozi wa Chadema UK. |
Brother Cobby akijiunga rasmi na Chadema. |
Mzee Makelele akimkabidhi kadi mwanachama mpya dada AZIZA. |
Mwenyekiti wa wanawake akiwahimiza akina mama kujiunga na M4C |
Baadhi ya wanachama wapya kwenye picha ya pamoja na viongozi |
Thursday, 13 September 2012
CHADEMA yafungua kesi mahakamani dhidi ya Nape; Yazungumzia inakopata ufadhili
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
kimekiri kufadhiliwa kutoka nje ya nchi katika shughuli zake za kujijengea
uwezo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS).
Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, CHADEMA na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini.
Dkt. Slaa alidai kuwa CHADEMA ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo.
“Kwa sasa kumekuwa na propaganda zinazoenezwa kwamba CHADEMA wanapata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili, hii si kweli, ila wanatujengea uwezo na si kutufadhili kampeni. Napenda kusema propaganda za aina hii zimepitwa na wakati na wote watakaozifanya tutawafungulia kesi,” alisema Dkt. Slaa.
“Wanaosema kwamba CHADEMA wanapokea mabilioni nao wanashirikiana na mashirika ya aina hiyo yenye mrengo mmoja na ni utamaduni duniani kote, vyama vyenye mrengo mmoja kushirikiana, hivyo hii dhana isipotoshwe,” alidai.
Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa CHADEMA kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dkt. Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.
Pia alisema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni.
Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dkt. Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa CHADEMA kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.
Nape ashitakiwa
Dkt. Slaa alidai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Slaa, tayari CHADEMA imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka CHADEMA kufadhiliwa kutoka nje.
Dkt. Slaa alisema kuwa, kesi hiyo yenye tuhuma zaidi ya tano, pia itawaunganisha watu wengine waliowahi kutamka kauli za namna hiyo vikiwamo vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo.
“CHADEMA tumeamua kumfikisha Nape mahakamani, ili atuthibitishie hayo mamilioni tunayopokea kwa wafadhili wa Ujerumani na kesi hii, itawaunganisha na wale waliowahi kusema kauli kama hiyo. Hapa mnaona kuna wageni, hawa ni viongozi kutoka Ujerumani na baadhi yao ni watumishi wa Serikali ya nchi hiyo, sasa tumekutana hapa kwa makusudi, ili kuwaeleza wazi jinsi wenzetu wanavyosema kutokana na ushirikiano wetu na wao. Tunashangaa sana, yaani CHADEMA ikishirikiana na watu kutoka nje ya nchi wanasema na kuzusha mambo ambayo yanaweza kuleta utengano kati ya nchi na taifa jingine. Kwa mfano, sisi CHADEMA tunashirikiana na Taasisi ya Korrad Adenauer Stiftung ya Ujerumani, CCM inashirikiana na FES, CUF inashirikiana na FNF zote za Ujerumani, sasa tunataka Nape atueleze mbele ya Mahakama juu ya jambo hili,” alisema Dkt. Slaa.
Dkt. Slaa alidai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.
Semina ya KAS
Akizungumzia semina ya kujenga uwezo iliyotolewa jana kwa makada wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema imelenga kuangalia wanavyoweza kuleta uchumi wa soko utakaoshirikisha watu walio katika ngazi za juu na chini.
Lengo la kushirikisha watu hao wa tabaka mbalimbali kwa mujibu wa Dkt. Slaa, ni ili raslimali za nchi zitumike kwa faida ya Watanzania wote ambapo pia mgeni kutoka KAS ambaye alipata kuwa Naibu Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich atatoa mada.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.
Mbowe pia alisema lengo la kukutana na mawaziri na wabunge wa Ujerumani jana ni kujadili masuala ya uchumi duniani na mahitaji yake katika nchi mbalimbali. Akasema chama cha siasa kinapaswa kutimiza majukumu yake, lakini pia kinapaswa kutambua kina wajibu wa kujadili uchumi wa taifa lake pamoja na utamaduni wa asili.
“Leo tumekutana na viongozi kutoka Ujerumani kubadilishana uwezo wa kisiasa, kujifunza kutengeneza vitabu, Katiba na mafunzo kwa viongozi. Lakini, nimetumia nafasi hii kuwaeleza hili la CCM na Serikali yake kutoa tuhuma kutufadhili jambo ambalo watalifanyia kazi kadiri watakavyoona. Pia tumewaeleza kwamba, Serikali hii inapokwenda kuomba msaada katika mataifa makubwa inasema inatekeleza sera na uchumi wa soko, lakini wanaporudi nyumbani wanawaeleza wananchi kuwa wanatekeleza ujamaa na kujitegemea jambo ambalo ni uongo. Sisi CHADEMA tupo pande zote, tunachagua yaliyo mazuri katika pande hizo na kuyafanyia kazi ili kuendana na soko huru, kuna misingi ambayo wakipewa watu binafsi wanaweza kusimamia uchumi, lakini hiyo isiondoe wajibu wa Serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi,” alisema.
Naye aliyekuwa Mbunge na Waziri wa Uchumi na Maendeleo katika Serikali ya Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich, alisema maendeleo ya nchi yoyote hayaji kama hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wakujitawala.
Alisema kwamba, ili wananchi wapate maendeleo ni lazima Serikali itoe fursa sawa ya kuwasikiliza wanachodai na kwamba, Tanzania inasifika kwa amani na utulivu lakini anashangaa kuwapo na malalamiko,” alisema.
Katika mazungumzo yake, alionyesha kutoridhishwa na kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Marehemu Daudi Mwangosi, aliyeuawa Iringa wakati akitekeleza wajibu wake.
Wavuti
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Willibrod Slaa alisema hayo jana katika semina iliyoshirikisha baadhi ya viongozi wa chama hicho na wageni kutoka shirika la Chama cha Kikristo cha Ujerumani (CDU) la Konrad Adenauer Stiftung (KAS).
Kwa mujibu wa Dkt. Slaa, CHADEMA na KAS, wamekuwa na ushirikiano wa karibu kwa miaka sita sasa na ushirikiano huo umelenga zaidi kukuza demokrasia nchini.
Dkt. Slaa alidai kuwa CHADEMA ni chama chenye uwazi kwa kila mtu na katika uhusiano wao na KAS, hakiletewi fedha moja kwa moja kwa ajili ya operesheni au maandamano, ila kujijenga kiuwezo.
“Kwa sasa kumekuwa na propaganda zinazoenezwa kwamba CHADEMA wanapata mabilioni ya fedha kutoka kwa wafadhili, hii si kweli, ila wanatujengea uwezo na si kutufadhili kampeni. Napenda kusema propaganda za aina hii zimepitwa na wakati na wote watakaozifanya tutawafungulia kesi,” alisema Dkt. Slaa.
“Wanaosema kwamba CHADEMA wanapokea mabilioni nao wanashirikiana na mashirika ya aina hiyo yenye mrengo mmoja na ni utamaduni duniani kote, vyama vyenye mrengo mmoja kushirikiana, hivyo hii dhana isipotoshwe,” alidai.
Pamoja na kusema kuwa KAS haitoi fedha moja kwa moja kwa CHADEMA kwa ajili ya maandamano na kampeni, lakini Dkt. Slaa alidai kuwa shirika hilo huwasaidia wastani wa Sh milioni 60 kwa mwaka kwa ajili ya machapisho na kutoa elimu.
Pia alisema kipo chama cha Uholanzi ambacho hakukitaja jina, lakini akakiri kuwa huwafadhili Sh milioni 20 kulingana na idadi ya wabunge walio bungeni.
Pamoja na kusema kuwa ni kawaida kwa vyama vya mrengo mmoja kusaidiana duniani, Dkt. Slaa alisema chama hicho cha Uholanzi kinachowasaidia, pia hufadhili CCM fedha zaidi ya zinazopelekwa CHADEMA kutokana na chama hicho tawala kuwa na idadi kubwa ya wabunge.
Nape ashitakiwa
Dkt. Slaa alidai kwamba kwa kuanzia wameamua kumshitaki Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Kwa mujibu wa madai ya Dkt. Slaa, tayari CHADEMA imefungua kesi namba 186 ya mwaka 2012, katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam dhidi Nape, ambaye anadaiwa alitamka CHADEMA kufadhiliwa kutoka nje.
Dkt. Slaa alisema kuwa, kesi hiyo yenye tuhuma zaidi ya tano, pia itawaunganisha watu wengine waliowahi kutamka kauli za namna hiyo vikiwamo vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo.
“CHADEMA tumeamua kumfikisha Nape mahakamani, ili atuthibitishie hayo mamilioni tunayopokea kwa wafadhili wa Ujerumani na kesi hii, itawaunganisha na wale waliowahi kusema kauli kama hiyo. Hapa mnaona kuna wageni, hawa ni viongozi kutoka Ujerumani na baadhi yao ni watumishi wa Serikali ya nchi hiyo, sasa tumekutana hapa kwa makusudi, ili kuwaeleza wazi jinsi wenzetu wanavyosema kutokana na ushirikiano wetu na wao. Tunashangaa sana, yaani CHADEMA ikishirikiana na watu kutoka nje ya nchi wanasema na kuzusha mambo ambayo yanaweza kuleta utengano kati ya nchi na taifa jingine. Kwa mfano, sisi CHADEMA tunashirikiana na Taasisi ya Korrad Adenauer Stiftung ya Ujerumani, CCM inashirikiana na FES, CUF inashirikiana na FNF zote za Ujerumani, sasa tunataka Nape atueleze mbele ya Mahakama juu ya jambo hili,” alisema Dkt. Slaa.
Dkt. Slaa alidai kuwa kesi hiyo itakapokuwa ikiendelea, wataongeza watu wengine walioeneza kauli hiyo.
Semina ya KAS
Akizungumzia semina ya kujenga uwezo iliyotolewa jana kwa makada wa CHADEMA, Dkt. Slaa alisema imelenga kuangalia wanavyoweza kuleta uchumi wa soko utakaoshirikisha watu walio katika ngazi za juu na chini.
Lengo la kushirikisha watu hao wa tabaka mbalimbali kwa mujibu wa Dkt. Slaa, ni ili raslimali za nchi zitumike kwa faida ya Watanzania wote ambapo pia mgeni kutoka KAS ambaye alipata kuwa Naibu Waziri wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich atatoa mada.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema ili uchumi uwe endelevu, lazima wananchi wapewe haki na kuruhusu sekta binafsi kusimamia uchumi na si rahisi kusimamia uchumi kwa sera za kijamaa.
Mbowe pia alisema lengo la kukutana na mawaziri na wabunge wa Ujerumani jana ni kujadili masuala ya uchumi duniani na mahitaji yake katika nchi mbalimbali. Akasema chama cha siasa kinapaswa kutimiza majukumu yake, lakini pia kinapaswa kutambua kina wajibu wa kujadili uchumi wa taifa lake pamoja na utamaduni wa asili.
“Leo tumekutana na viongozi kutoka Ujerumani kubadilishana uwezo wa kisiasa, kujifunza kutengeneza vitabu, Katiba na mafunzo kwa viongozi. Lakini, nimetumia nafasi hii kuwaeleza hili la CCM na Serikali yake kutoa tuhuma kutufadhili jambo ambalo watalifanyia kazi kadiri watakavyoona. Pia tumewaeleza kwamba, Serikali hii inapokwenda kuomba msaada katika mataifa makubwa inasema inatekeleza sera na uchumi wa soko, lakini wanaporudi nyumbani wanawaeleza wananchi kuwa wanatekeleza ujamaa na kujitegemea jambo ambalo ni uongo. Sisi CHADEMA tupo pande zote, tunachagua yaliyo mazuri katika pande hizo na kuyafanyia kazi ili kuendana na soko huru, kuna misingi ambayo wakipewa watu binafsi wanaweza kusimamia uchumi, lakini hiyo isiondoe wajibu wa Serikali kutekeleza wajibu wake kwa wananchi,” alisema.
Naye aliyekuwa Mbunge na Waziri wa Uchumi na Maendeleo katika Serikali ya Ujerumani, Klaus-Jurgen Hedrich, alisema maendeleo ya nchi yoyote hayaji kama hakuna uhuru wa kutoa maoni na uhuru wakujitawala.
Alisema kwamba, ili wananchi wapate maendeleo ni lazima Serikali itoe fursa sawa ya kuwasikiliza wanachodai na kwamba, Tanzania inasifika kwa amani na utulivu lakini anashangaa kuwapo na malalamiko,” alisema.
Katika mazungumzo yake, alionyesha kutoridhishwa na kifo cha Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Channel ten, Marehemu Daudi Mwangosi, aliyeuawa Iringa wakati akitekeleza wajibu wake.
Wavuti
MH. JOHN MNYIKA NA MAJIBU YA TANESCO KUHUSU UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA FIDIA KWA WANANCHI WANAOISHI MAENEO HATARISHI YA KARIBU NA MITAMBO YA KUFUA UMEME UBUNGO
SIJARIDHIKA NA MAJIBU YA TANESCO KUHUSU UCHAFUZI WA MAZINGIRA, FIDIA YA WANANCHI WANAOISHI MAENEO HATARISHI YA KARIBU NA MITAMBO YA KUFUA UMEME UBUNGO IHARAKISHWE
Tarehe 9 Septemba 2012 baadhi ya vyombo vya habari viliandika habari kwamba wakazi zaidi ya 500 wa eneo la Ubungo Darajani karibu na Riverside wanalalamika kuishi kwenye mfereji wa maji taka wenye mafuta ya mitambo na mchanganyiko wa kemikali kadhaa zinazodaiwa kuzalishwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Sijaridhika na majibu yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Felichism Mramba kwamba shirika hilo limedhibiti mfumo wa maji taka na haihusiki na tatizo hilo la kuchafua makazi na mazingira.
Kufuatia kauli hiyo, natoa wito kwa Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO kutoa majibu ya wazi kwa wananchi ni kampuni gani hasa inahusika na uchafuzi huo wa mazingira na kuchukua hatua zinazostahili kurekebisha mfumo uliopo.
Ikiwa hatua hazitachukuliwa nitaungana na wananchi kufikisha malalamiko yao kwenye mamlaka zinazohusika na usimamizi wa mazingira katika Manispaa ya Kinondoni na katika Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri wa Nishati na Madini na Kaimu Mkurugenzi wa TANESCO watoe majibu ya wazi kwa wananchi ni lini fidia ya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayozunguka mitambo ya kuzalishia umeme ya Ubungo itaanza kulipwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 kutokana na kiasi cha shilingi bilioni 10 ambacho tayari kimeshaingizwa kwenye bajeti.
Izingatiwe kwamba tarehe 04 Aprili 2012 nilifanya mkutano na wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama wamachinga zaidi ya 500 katika kata ya Ubungo ambapo pamoja na mambo mengine nilitoa siku tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO kueleza hatua walizochukua katika kutekeleza ahadi waliyoniahidi kwa nyakati mbalimbali kwenye mwaka wa fedha 2011/2012 wakati wa vikao vya kamati ya nishati na madini nilipohoji kuhusu hatma ya wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi jirani na mitambo ya umeme ikiwemo kuhusu uchafuzi wa mazingira unaoendelea.
Ikumbukwe kwamba mwaka 2004 baada ya mitambo kulipuka serikali iliahidi kuwalipa fidia wananchi husika na kuwahamisha, mwaka 2009 Serikali ikarudia tena ahadi hiyo lakini mpaka tarehe 4 Aprili 2012 ilikuwa haijatekelezwa hata kwa mtu mmoja.
Ndani ya siku hizo tatu, TANESCO ilitoa ahadi ya kuwa suala la fidia kwa wananchi litaingizwa katika bajeti ya serikali mapema iwezekanavyo na tayari kiasi cha shilingi bilioni 10 kimetengwa kwa ajili ya kuanza kulipa fidia ikiwa ni sehemu ya Mradi wa Kuboresha Mifumo ya Umeme Katika Jiji la Dar es salaam (Kasma 3154).
Ili kuhakikisha kwamba mpango wa kulipa fidia ikiwa ni sehemu pia ya kuboresha mazingira ya eneo husika tarehe 27 Julai 2012 katika hotuba yangu bungeni kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani niliitaka Wizara ya Nishati na Madini ieleze iwapo kiasi cha 10,000,000,000 kilichotengwa kwa ajili ya kulipa fidia wananchi wanaoishi katika maeneo hatarishi yanayozunguka mitambo ya kuzalishia umeme ya Ubungo kitatosha kukamilisha kazi hiyo kwa mwaka wa fedha 2012/2013 ili kuepusha uwezekano wa gharama kuongezeka kutokana na riba ya kuchelewa kufanya malipo kama ilivyotokea kwa miaka iliyopita.
John Mnyika (Mb)
09 Septemba 2012
Thursday, 6 September 2012
CHADEMA waikataa tume ya Nchimbi
TENDWA AIBUKA, ATISHIA
KUWAFUTIA USAJILI
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), kimeipinga tume ya kuchunguza mauaji ya aliyekuwa mwandishi
wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, iliyoundwa na Waziri wa Mambo wa Ndani, Dk.
Emmanuel Nchimbi, kwa maelezo kuwa inaongozwa na jaji asiye na
sifa.
Kimesema kuwa Jaji huyo
mstaafu, Stephen Ihema, anafahamika ni mtu asiyejua kazi, kwani ameshindwa kutoa
hukumu katika kesi zaidi ya 300.
Akizungumza na waandishi
jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za
Binadamu wa chama hicho, Tundu Lissu, alisema kutokana na Jaji Ihema kutoweza
kazi, hata Jaji Bernard Luanda alipata kumkosoa kwa kutoa waraka kwa majaji wote
mwaka 2005.
“Kama mnafuatilia taarifa
za hivi karibuni, Ihema ni mmoja wa majaji waliopo kinyume cha sheria na Katiba.
Aliteuliwa kuwa jaji enzi za Benjamin Mkapa, ilipofika mwaka 2003 kwa sababu
hakuwa anajua sheria,” alisema.
Lissu ambaye ni Mbunge wa
Singida Mashariki, aliongeza kuwa Ihema hajui kazi ya ujaji na kwamba
alisharundika zaidi ya kesi 300 ambazo anashindwa kuziandikia hukumu. Na kuwa
mtu ambaye anajulikana kutokuwa na uwezo wowote wa kufanya kazi ya
kisheria.
“Ndugu zangu na hili naomba
nirudie maana wasiseme tumeanza maneno yetu, mwaka 2003 kabla mimi sijawa mbunge
kuna mtu anaitwa Joram Alute, ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Singida kwa sababu
ya ubovu wa Jaji Ihema, Joram alimwandikia Rais Mkapa barua ya kumuomba
kumuondoa Jaji Ihema Mahakama Kuu, kwa sababu hakuwa na uwezo wowote wa kufanya
kazi ya ujaji.
Miaka karibu 10 wana CCM,
Joram Alute, si CHADEMA, alisema hawezi kazi, aidha ni mvivu au hajui namna ya
kuandika hukumu, hafai kuwa jaji,” alisema Lissu.
Aliongeza kuwa mwaka 2005
Jaji Ihema alikuwa amemaliza mkataba wa kwanza na kupewa mwingine wa kazi ya
ujaji, hali ambayo ilimfanya Jaji Bernard Luanda (sasa Jaji wa Mahakama ya
Rufaa), baada ya kuandikiwa na Jaji Manento kuwa Ihema amepewa mkataba wa ujaji,
aliandika waraka uliosambazwa kwa majaji wote kuwa Ihema si jaji kwa mujibu wa
Katiba.
Alisema kwa mujibu wa
sheria za nchi, majaji wanateuliwa, hivyo Jaji Ihema kupewa mkataba ni kinyume
cha sheria na katiba.
Lissu alieleza kuwa hata
alipopelekwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, tume hiyo ilikuwa ni ya
kuficha uchafu na madhambi ya viongozi, kwani ilikuwa kimya kwa miaka yote huku
viongozi wakishiriki kufilisi taifa.
Alisema kutokana na maelezo
hayo ni dhahiri kuwa Ihema hana uwezo na pia maadili yake ni ya mashaka, kwani
hilo linafahamika ndani ya mahakama.
Pamoja na hilo, alisema
tume hiyo imeundwa kwa lengo la kurekebisha mambo baada ya Jeshi la Polisi
kukamatwa mchana kweupe wakifanya mauaji.
“Ni tume ambayo lengo lake
si kuchunguza mauaji, ni kuondoa hii picha ya mauaji yaliyofanywa na Jeshi la
Polisi hadhaharani…hii ndivyo tunavyoiangalia.
Kwa kuwa si tume ya
kuchunguza mauaji sisi kama chama hatutaiunga mkono na tutawashauri wananchi wa
Tanzania, wawe wanachama wetu, wasiwe wanachama wetu, wasiiunge mkono,”
alisema.
Nchimbi
akosolewa
Lissu alisema kwa mujibu wa
sheria ya kuunda tume za uchunguzi mwaka 1962 sura ya 29, anayepaswa kuunda tume
ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kutoa hadidu rejea na kwamba
kulingana na utaratibu huo si jukumu la waziri kuunda tume.
Alisema tume za aina hiyo
zinatoa ripoti kwa rais au zinaweza kutoa taarifa hadharani endapo rais
ataelekeza hivyo katika hadidu rejea.
“Hivyo kwa matukio makubwa
ya kitaifa yanayotokea, kisheria ni jukumu la rais, si jukumu la waziri ambaye
anawasimamia watuhumiwa wa hicho kinachotakiwa kuchunguzwa.
Kwa hiyo katika upeo huo wa
kisheria, Waziri Nchimbi hana mamlaka ya kuunda tume ya kuchunguza mauaji hayo,”
alisema.
Lissu alifafanua kuwa
walioua ni polisi ambao inawezekana waliamriwa waue na wakubwa zao kisiasa
(waziri) au kiutendaji (IGP na maofisa wengine wa jeshi), hivyo kama unachunguza
mauaji yaliyofanyika waziwazi, inawezekana yamefanywa kwa amri za kisiasa au
kiutendaji.
Hivyo alihoji kama tume
hiyo ina uwezo wa kumhoji waziri au IGP na kusema kuwa: “Tume hii ni danganya
toto, ya kitchen party, pengine na ya marafiki, ili kuondoa picha mbaya kwa
Jeshi la Polisi,” alisema.
Wajumbe wake
waguswa
Lissu alisema Naibu
Kamishna wa Polisi, Isaya Mungulu, kutoka makao makuu hana uwezo kwa kumuita
waziri au IGP kwa ajili ya kumhoji kuhusiana na mauaji hayo.
Kuhusu mtaalamu wa mabomu,
Wema Wapo, kutoka Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ) alihoji kuwa
anakwenda kuchunguza kitu gani kisichojulikana, kwani katika picha muuaji
anajulikana.
“Inaonekana ni bomu la
machozi ambalo alipigwa nalo, ambalo limemchanachana. Sasa ni kitu gani
kisichojulikana. Sasa unaita mtaalamu achunguze mlipuko upi ambao haujulikani?”
alihoji.
Kwa upande wa Theopili
Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri (TEF) na Pili Mtambalike kutoka Baraza la
Habari Tanzania (MCT), alisema hao ni waandishi wa habari na kuhoji iwapo wana
utaalamu wa kuchunguza vifo.
“Hii ni tume ya marafiki,
yenye lengo la kukosha mauaji yaliyofanywa na marafiki, kwa vyovyote vile hii si
tume halali ya kuchunguza mauaji ya Mwangosi,” alisema Lissu.
Hadidu rejea
zapingwa
Lissu alihoji ni mtu gani
asiyefahamu chanzo cha mauaji hayo, kwani vyombo vya habari vimemuonyesha
kupitia picha, hivyo kuhoji tume hiyo inakwenda kuchunguza kitu
gani.
Kuhusu swali kama kweli
kuna uhasama kati ya polisi mkoani Iringa na waandishi, alihoji iwapo tume hiyo
inakwenda kuchunguza mauaji ama uhasama.
Kwa upande wa swali kama
nguvu iliyotumika na polisi ilikuwa sahihi, alisema kuwa hilo ni suala la
kisheria na pia kunahitajika ushahidi.
“Kuhusu swali linalohoji
mahusiano kati ya polisi na vyama vya siasa. Hili liko wazi kabisa kwa sababu
sijawahi kusikia Jeshi la Polisi limevunja mikutano ya CCM, kwa hiyo hapa
wanakwenda kuichunguza CHADEMA,” alisema.
Aliongeza kuwa iwapo
wanataka kuchunguza suala hilo kwa nini Mungulu yupo kwenye tume hiyo na hakuna
mtu wa CHADEMA wala Msajili wa Vyama vya Siasa au mwakilishi wake.
“Hii si tume ya kuchunguza
mauaji, ni ya kufunika mauaji haya…hatuwezi kukubaliana na tume hii,”
alisema.
Mbali na hilo, alisema kuna
haja ya kuchunguza matukio mbalimbali ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni
likiwemo la Morogoro, Arusha, Igunga na Arumeru Mashariki.
“Matukio yote haya
hayajachunguzwa inavyostahili. Hatutaki mambo yaishe hivi hivi,”
alisema.
Mapendekezo
yao
Kutokana na hali hiyo,
alisema chama hicho kinamtaka Rais Jakaya Kikwete kuunda tume ya uchunguzi wa
mauaji ambayo itaongozwa na majaji waadilifu na kwamba itakuwa bora iwapo
watatoka Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu, ambao watafanya uchunguzi wa
wazi.
“Katika tume hiyo mashahidi
watakuwa wakiitwa hadharani. Tume za aina hii hazipo, lakini kwa mujibu wa
sheria Rais anaweza kuunda tume hiyo. Hatutaki uchunguzi wa kificho ambao
unaonesha polisi hawakukosea,” alisema.
Alieleza kuwa tume hiyo
itakuwa na mamlaka ya kumuita mtu yeyote isipokuwa rais. Na kwamba kwa kuwa
muuaji anajulikana, chama hicho kinataka askari wote waliohusika wakamatwe na
kufunguliwa kesi ya mauaji.
“Tunajua si wote walioua,
ila katika sheria kuna kitu kinaitwa common intension, mmoja ameua, lakini
alioshirikiana nao wanahusika. Hili linawezekana kwa kuwa kuna ushahidi,”
alisema.
Alisema iwapo rais hataunda
tume hiyo, kuna njia nyingi za kuendelea na suala hilo, na kusema hilo chama
kinapaswa kutoa kauli.
Wataka Nchimbi
ajiuzulu
Katika hatua nyingine,
Lissu alisema kutokana na tukio hilo, Waziri Nchimbi anapaswa kuwajibika kisiasa
kwa kujiuzulu, kwani hawezi kuendelea kuwa waziri na kuheshimika kutokana na
tukio hilo.
“Kama ana chembe ya
uadilifu afuate nyayo za Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi) miaka 36 iliyopita ambaye
alijiuzulu uwaziri. Nchimbi hawezi kuwa waziri na kuendelea kuheshimika kama
anaongoza jeshi la wauaji. Akishindwa kujiuzulu rais amfukuze kazi,”
alisema.
Alieleza kuwa mauaji ya
aina hiyo ni ya kisiasa na kuongeza kuwa jeshi hilo limekuwa likifanya kazi kwa
niaba ya CCM.
Tendwa
aibuka
Mauaji ya Daudi Mwangosi,
anayedaiwa kuuawa kwa bomu na askari polisi mkoani Iringa, yamemuibua Msajili wa
Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, ambaye ametishia kuvifuta vyama
vinavyojihusisha na siasa za vurugu.
Katika mkutano wake na
waandishi wa habari jana, Tendwa ambaye alitumia muda mwingi kuwatisha CHADEMA
pia amelionya Jeshi la Polisi na kulitaka lifanye kazi zake kwa wajibu wa sheria
za nchi.
Tendwa ambaye ofisi yake
imekuwa ikilalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa inashindwa kutekeleza wajibu
wake kutokana na kuegemea upande wa Chama tawala cha CCM, alisema kuwa
demokrasia ya sasa imekua na kusababisha vifo vya raia wasio na
hatia.
Alisema hawezi kuvumilia
siasa za vurugu zinazohatarisha amani ya taifa lililopata uhuru wake miaka 50
iliyopita kwa kisingizio cha operesheni za ukombozi.
Tendwa alisema haoni haja
ya CHADEMA kuendelea na operesheni yao ya Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) wakati
huu ambao si kipindi cha uchaguzi, hivyo kutishia kukifuta chama hicho alichodai
mikutano yake imekuwa ikizusha vurugu.
Aliainisha kuwa kuanzia
mwaka jana hadi sasa mauaji kadhaa ya raia yametokea katika mikutano ya kisiasa
katika mikoa ya Arusha, Singida, Morogoro na Iringa na kwamba hali hiyo
haiwezekani kusema taifa ni huru.
Alisema kuwa Agosti 10
mwaka huu, mkutano wa vyama vya siasa na Jeshi la Polisi ulifanyika na
kuzungumzia masuala mbalimbali likiwamo la amani nchini, kufanyika kwa mikutano
ya vyama, wajibu wa vyama vya siasa kwa kufuata sheria za nchi na wajibu wa
Jeshi la Polisi nchini.
Tendwa aliongeza kuwa
kutokana na kuwapo kwa sheria ya mikutano ya vyama vya siasa nchini, ikitokea
chama chochote cha siasa kitaleta chuki na uvunjifu wa amani kitapaswa
kufutwa.
“Kutokana na hali
tuliyoifikia kwa sasa inatisha, hivyo vyama vya siasa viondoe uchochezi,”
aliongeza.
Pia amelitaka Jeshi la
Polisi kutimiza wajibu wake wa kulinda raia pamoja na mali zao na kuwataka
wavitumie vyombo vyao kwa ustaarabu.
DCI asuswa
Iringa
Jeshi la Polisi nchini
limeanza kuonja shuluba ya matukio yao kususiwa na waandishi wa habari, ambapo
jana Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai nchini, DCI Robert Manumba, alikuwa wa kwanza
kukumbwa na adha hiyo mkoani Iringa.
Waandishi wa habari
wameazimia kutoripoti taarifa zozote za jeshi hilo hadi hapo wale waliohusika
katika kusababisha kifo cha mwanahabari, Daudi Mwangosi, watakapokuwa
wamekamatwa na kuchukuliwa hatua.
Manumba ambaye jana alikuwa
akitaka kutoa taarifa za awali juu ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi, alijikuta
katika wakati mgumu baada ya wanahabari hao kugoma kabisa kwenda
kumsikiliza.
Pia waandishi hao wamekosoa
tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi,
wakisema haijakidhi haja wala kuzingatia uwiano, kwa kile walichoeleza kuwa
hakuna hata klabu moja ya waandishi wa habari iliyoshirikishwa.
Awali waandishi hao walitoa
masharti kwa DCI wakitaka awepo peke yake katika chumba cha mikutano lakini
Manumba alijitetea kuwa tamko alilotaka kutoa ni lazima na maofisa hao
walisikie.
“Jamani punguzeni jazba juu
ya hili, ninajua mna mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa hili na suala hili
limemgusa kila mmoja, hasa ninyi waandishi wa habari, hivyo naomba mnisikilize
na mjue tunataka kuwaambia nini,” alisema DCI Manumba bila
mafanikio.
Wakati huo huo, waandishi
wa habari mkoani hapa, walisema wakati tume iliyoundwa na Dk. Nchimbi haijaanza
kazi yake rasmi ni vema Kamanda wa Polisi mkoani humo akaachia madaraka yake kwa
muda ili kupisha uchunguzi huru.
Katibu wa Chama cha
Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa, Frank Leonard, alisema mbali na kumtaka
Kamuhanda kujiuzulu pia ni wakati muafaka kwa tume iliyoundwa ikawahusisha na
viongozi wa klabu ya waandishi.
TUCTA yamlilia
Mwangosi
Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Nchini (Tucta), limemlia aliyekuwa mwandishi wa kituo cha runinga
cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi, likisema alikuwa ni mchapa
kazi.
Katibu Mkuu wa Tucta,
Hezron Kaaya, alisema kuwa ni jambo la kusikitisha na kushangaza kwa mwandishi
kuuawa wakati akitekeleza majukumu yake.
“Kwa kweli Tucta kati ya
mambo ambayo yametuuma na kutusikitisha ni kifo cha Mwangosi kinachoripotiwa
kufanywa na Jeshi la Polisi, hasa kitendo cha kusambaratishwa mwili wake, kwani
hata mnyama anapouawa katika mawindo huwa hauawi kwa namna ile,”
alisema.
Kaaya aliongeza kuwa ni
jambo la kusikitisha kwa kuwa kifo kile kitachukua muda mrefu kwa Watanzania
kukisahau kwani hakuwa na kosa lolote alilolifanya mpaka kuuawa namna
ile.
Aliongeza kuwa kwa hali
ilivyo sasa taifa linaelekea pabaya, kwa sababu haki ya mnyonge haizingatiwi
tena na wenye nguvu, akitoa mfano kuwa wanyonge wanapodai haki yao jibu rahisi
ni kusambaratishwa kwa mabomu na virungu vya polisi.
Alisema endapo hali hiyo
itaachwa iendelee hivyo, kunaweza kutokea maafa makubwa kwa wananchi waliochoka
kuonewa na kudhulumiwa haki zao.
Kaaya alibainisha kuwa
Watanzania wengi wameuawa katika matukio ya kisiasa na hakuna hatua madhubuti
zilizochukuliwa kukomesha hali hiyo isiendelee kutokea, badala yake zinaundwa
tume ambazo hata hivyo hazijulikani zinakoishia zaidi ya kutumia fedha za walala
hoi.
Tanzania Daima
Tanzania Daima
Tuesday, 4 September 2012
CHADEMA UK KUUNGURUMA MILTON KEYNES
BAADA YA KUISAMBARATISHAccm READING, WIMBI LA MABADILIKO YA LAZIMA SASA KUUNGURUMA MILTON KEYNES
TAWI LA UK
TUNAWATANGAZIA WATANZANIA WOTE WAISHIO MILTON KEYNES NA MIJI YA JIRANI
KUWA KUTAKUWA NA MKUTANO UTAKAOFANYIKA
TAREHE 15/09/2012 KUANZIA SAA SABA MCHANA MPAKA SAA KUMI NA MBILI JIONI
TUTAWAJULISHA BAADAE KUHUSU UKUMBI
MNAKARIBISHWA MJIUNGE NA HARAKATI ZA KUENEZA DEMOKRASIA YA KWELI NCHINI KWETU
HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE
SISI SOTE NI NDUGU TATIZO NI CCM
Kutakuwa na usafiri kutoka London na Reading
REFRESHMENTS WILL BE AVAILABLE
kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na wafuatao:-
Mwenyekiti: Mr CHRIS LUKOSI - 07903828119
&
Mwakilishi wa Reading: Mr GERALD LUSINGU
PEOPLE'S POWER
Sunday, 2 September 2012
Matukio mbalimbali katika mkutano wa M4C Reading
Mwenyekiti Mh Likosi Akihutubia Mkutano |
Katibu wa Chadema UK Kamanda Liberatus Musiba akiwa na Mwenyekiti wakifuatilia mkutano |
Mh Lukosi na Mweka Hazina Dr Alex wakimsikiliza kwa makini Kamanda Godbless Lema akihutubia mkutano huo kwa njia ya simu |
Dr Alex Paurine ambaye pia ni Mweka hazina akihutubia mkutano huo, Dr Paurine alitumia Power Point kuonyesha picha na matukio yanayoonyesha hali halisi ya maisha ya Watanzania wengi. |
Ndg Aseri Katanga Mwenyekiti wa bodi ya Computer for Africa akihutubia |
Gerald Lusingu, Mmoja wa wenyeji wa Mkutano wa M4C Reading na aliyechaguliwa kuwa mwakilishi wa M4C Reading akiwasalimia wananchi |
Dr Lusingu akitoa Historia ya Harakati za Mabadiliko na Mageuzi katika nchi yetu, huku akifuatiliwa kwa makini na Katibu wa wanawake Bi Margaret Malekia, Katibu Mh Liberatus na Mwenyekiti Mh Lukosi |
Engineer Prudence Kahatano akichambua matokeo ya azimio la Zanzibar lililovunja azimio la Arusha na madhara ya soko huria kwa Watanzania |
Wadau Mbalimbali katika Mkutano
Wanachama mbali mbali wakikabidhiwa kadi za Chadema na Mwenyekiti wa Chadema UK Mh Chriss Lukosi
Ndg Wambura akivalishwa Gwanda na Kupewa kadi ya Chadema na Mwenyekiti Mh Lukosi |
Saturday, 25 August 2012
TAARIFA YA USAFIRI KWENDA M4C READING
TAWI LA CHADEMA UK LINAPENDA KUWATANGAZIWA WANACHAMA WAKE WOTE, WATANZANIA WOTE NA WAPENZI WA CHADEMA WAISHIO LONDON KUWA WAWASILIANE NA CHRIS LUKOSI KWA TARATIBU ZA USAFIRI WA KWENDA READING KUHUDHULIA MKUTANO WA M4C.
MAGARI YATAONDOKA SAA NNE ASUBUHI
Mkutano utafanyika siku ya Tarehe 26/08/2012 kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbili jioni, siku ya Bank Holiday. Risc Reading International Solidarity Centre, 35-39 London Street, Reading, RG1 4PS .
WASOMI WENGI NA WANAHARAKATI MBALI MBALI WATAONGEA SIKU HIYO,
SIKU YA MKUTANO TUTAANZISHA MFUKO WA KUFA NA KUZIKANA KWA AJILI YA WATANZANIA WOTE WAISHIO UK BILA KUBAGUA CHAMA CHAKO CUF,CCM,UDP,TLP WOTE MNAKARIBISHWA
Watanzania wote na wadau mbali mbali mnakaribishwa
SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO NI CCM
ni wakati wa kusimama na kusema tumechoka
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA HAWA WAFUATAO
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119
Au tutumie email kupitia chademauk@gmail.com
Peooooople's Power
Friday, 24 August 2012
Dk. Slaa: CCM wana sababu za kikoloni
KATIBU Mkuu wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), kinachukiwa na wananchi kutokana na kuendelea kujitetea kwa
kutumia sababu zilizotumiwa na wapigania uhuru wa Tanganyika kujikomboa katika
mikono ya wakoloni.
Akizungumza katika mikutano
ya hadhara kwenye vijiji mbalimbali vya kata za Ngerengere na Makambarai, Dk.
Slaa alisema serikali ya CCM imeshindwa kutengeneza fursa ya wananchi kujiletea
maendeleo yao licha ya kuwa katika nchi yenye rasilimali nyingi.
“Mwalimu Nyerere pamoja na
wapigania uhuru wengine wa Tanganyika hawakumkataa mkoloni kwa sababu ya rangi,
dini wala hali zao isipokuwa waliwakataa kwa vile walishindwa kuwaondolea watu
umaskini, ujinga na maradhi ambayo yanaendelea kutuandama kila wakati,”
alisema.
Alisema kuwa hayati Mwalimu
Nyerere alifikia malengo kwa kuonesha njia ya kupita, hivyo waliomfuatia
walikuwa na wajibu wa kuhakikisha njia hiyo inapitika lakini serikali ya CCM
imeamua kuziba njia hiyo.
Huku akisoma takwimu za
maendeleo katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, linaloongozwa na Dk. Lucy
Nkya (CCM), Dk. Slaa alisema kuwa hakuna sababu ya kuendelea kukivumilia chama
hicho kwa sababu ya kufanana kwa rangi na badala yake wananchi wanapaswa
kuchukua hatua ya kukipumzisha.
“Kila mmoja hapa amesikia
takwimu nilizosoma, tena zinatokana na vitabu vya serikali yenu hii mliyoichagua
na kuiweka madarakani, mlichagua rais wa CCM, mbunge wa CCM, Diwani wa CCM,
mwenyekiti wa kijiji na serikali ya kijiji ya CCM, sasa nawasomea hapa ufisadi
unaofaywa mnaanza kusikitika,” alisema.
Alisema ni aibu miaka 50
baada ya Uhuru kusikia Watanzania wakizungumzia upungufu wa madawati wakati nchi
nyingine zikiwa zinashindana kwenda kuangalia uwezekano wa kufanya utafiti
utakaozisaidia nchi zao.
Thursday, 23 August 2012
Mwalimu mmoja wanafunzi 652
Akiwa katika Oparation Sangara inayoendelea hivi sasa nchini, Mwenyekiti wa Baraza la vijana la Chadema, Bwana Deogratias Munishi amegundua shule ambayo inawanafunzi 652 na Mwalimu mmoja tu. Shule hiyo ipo katika Kijiji cha Kadodo Kata ya Luale, Mvomelo Mkoani Morogoro. Hii ndo hali halisi ya elimu Tanzania baada ya miaka 50 ya uhuru, chini ya utawala wa CCM.
Mwenye shati la rangi ya udongo na suruali nyeusi ndiye Mwalimu Mkuu na Mwalimu pekee wa Shule ya Msingi Kododo iliyopo kata ya Luale, Mvomelo Mkoani Morogoro. Shule hiyo inawanafuzi 652. |
Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa CCM kata ya Muhonda akieleza jinsi alivyokunwa na sera za CHADEMA zilizoelezwa na katibu Mkuu wa BAVICHA katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kichangani. |
Wednesday, 22 August 2012
Dr. Slaa na Rasilimali za Taifa
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dr Wilbrod Slaa amelitaka Jeshi la Polisi kutumia fedha na uwezo wake kulinda Rasilimali za Taifa sio kupambana na CHADEMA
Tuesday, 21 August 2012
MAHAKAMA YATENGUA UBUNGE JIMBO LA IGUNGA
Tuesday, 14 August 2012
CHADEMA KUWASHA MOTO KATIKA MJI WA READING SIKU YA TAREHE 26/08/2012
UK
Ili kufikia malengo
yetu ya kuzunguka kwenye Miji mbalimbali ya UK kuhamasisha Watanzania waishio
uk kujiunga na Chadema, kueneza kampeni ya m4c na kufungua matawi mengine, Tawi la
Chadema London linapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio katika Mji wa
Reading na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa M4C UK utakao fanyika Tarehe
26/08/2012 siku ya Bank holiday.
Dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha Watanzania
waishio UK kujiunga na chama, kushiriki katika harakati za mabadiliko, kusajili
wanachama wapya, kuchagua wawakilishi wa
muda kutoka mji wa Reading pamoja na kuanzisha mfuko wa kufa na kuzikana kwa manufaa
ya watanzania wote.
Tumekusudia
kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa sababu mpaka hivi sasa Mtanzania
akifariki akiwa UK hakuna taasisi wala
ofisi yoyote inayotoa msaada. Jukumu ambalo kwa muda mrefu Serikali yetu
kupitia ubalozi umelipuuzia na kushindwa kulisimamia na kulishughulikia.
Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.
Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.
Pia katika mkutano huo wanachama mbalimbali wa CCM walio na uchungu na nchi yetu na wanaopenda maendeleo na mabadiliko
ya kweli watapewa nafasi ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama
sehemu moja wapo ya kampeni yetu ya
Kuvua Gamba na Kuvaa Gwanda ukiwa Ughaibuni.
Mkutano utafanyika
siku ya Tarehe 26/08/2012, Kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbii jioni.
Risc Reading International
Solidarity Centre,
35-39 London Street,
Reading, RG1 4PS
Huu ndio wakati wa mabadiliko, kusimama na kusema tumechoka!
KWA
MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA;
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119,
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119,
Subscribe to:
Posts (Atom)
Chadema UK Ndani ya Milton Keynes
DAR NI SISI - VIDEO MAISHA YA WANADAR HATA BAADA YA MIAKA50 YA UHURU
