Monday 13 August 2012

MATUKIO MBALI MBALI KATIKA SIKU YA UFUNGUZI WA TAWI LA CHADEMA LONDON

VUA GAMBA VAA GWANDA UGAIBUNI

Katika Ufunguzi wa Tawi la CHADEMA London Wanachama mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi walijitokeza kurudisha kadi za CCM na kujiunga rasmi na CHADEMA. Wanachama hao walikabidhiwa kadi za uanachama na Mhe. Lema Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Taifa katika Kampeni Maalumu ya Vua Gamba Vaa Gwanda ukiwa Ugaibuni, Ili kuwapa nafasi watanzania waishio nje ya nchi kulivua Gamba, kuleta mabadiliko , kushiriki katika siasa, na harakati za kulikomboa Taifa kutoka katika utawala wa kifisadi, onyonyaji, uonevu na ahadi za uongo za CCM.


Mhe. Lema na Mwenyekiti wa Muda wa Chadema Lodon Chriss Lukosi wakionyesha baadhi ya kadi na Tshirt zilizorudisha na wanachama wa CCM
Mmoja aliyekuwa Mwanachama na Mkereketwa wa CCM toka Mwaka 1984 Ndg. Christopher Chegula akirudisha Tshirt na Kadi ya CCM kwa Mhe. Lema
Mhe. Lema akimkabidhi kadi ya Uanachama wa CHADEMA Christopher Chegula

Bi. Jessca Maduhu akipokea kadi ya uanachama wa chadema kwa furaha kutoka kwa Lema

Mwanachama Mpya akikabidhiwa kadi yake

Jessica akipokea kadi yake ya CHADEMA

Mmoja ya wanachama waliokabidhiwa kadi na Mh Lema

Esther baby Cuthbert akionyesha kadi yake mpya ya Chadema






WANACHAMA NA WADAU MBALIMBALI KATIKA MKUTANO
Kamanda Godbless Lema akiongea machache wakati  wa uzinduzi

Mwenyekiti Chris Lukosi akimtambulisha  Ndg. Magabe Mwanachama wa siku nyingi wa chadema UK

Baadhi ya waheshimiwa wakimsikiriza na kumfuatilia kamanda Lema kwa makini

Wanachama wa chadema wakifuatilia mkutano kwa makini


Baadhi ya wanachama waanzilishi wa tawi katika picha ya pamoja na Kamanda Lema

Lema na baadhi ya waheshimiwa waliohudhuria ufunguzi wa tawi wakibadilishana mawazo.

Mmoja wa wanachama wa Chadema akitoa maoni yake

Joe Kazi na Kamanda Lema Baada ya Mkutano


VIONGOZI WA MPITO WALIOCHAGULIWA KULIONGOZA TAWI LA CHADEMA LONDON

Mkutano wa ufunguzi wa Tawi la Chadema London ulikwenda sambamba na uchaguzi wa viongozi wa mpito wa Tawi watakao ratibu na kusimamia shughuli mbalimbali za chama kwa muda, uchaguzi uliongozwa na kusimamiwa na Mh Godbess Lema ambaye ni mjumbe wa Baraza Kuu la Chadema Taifa.
Viongozi waliochanguliwa kuratibu na kuongoza shughuli za chama kwa muda ni wafuatao;

Chris Lukosi - Mwenyekiti


Liberatus Musiba- Makamu Mwenyekiti
Christopher Chegula - Katibu Mwenezi
Dr. Alex Paurine- Mweka hazina
E.R. Lunyama - Katibu wa Vijana
Bi Jessca Maduhu- Mwenyekiti Baraza la Wanawake
Margaret Malekia- Katibu Baraza la Wanawake
Rodwell Lugano

Chris Swai- Think Tank Team Member

Archie Mbade- Think Tank Team Member



Viongozi wengine waliochanguliwa ni paomja Johnstone Malunda Mwenyekiti wa Vijana na Bw. Edmund Marealle aliyechaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu

No comments:

Post a Comment

Chadema UK Ndani ya Milton Keynes

DAR NI SISI - VIDEO MAISHA YA WANADAR HATA BAADA YA MIAKA50 YA UHURU