Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande ameahirisha
kesi ya rufaa ya aliyekuwa mbunge wa Arusha Mjini, hadi Oktoba 2, 2012 kwa
mujibu wa maombi ya mawakili wa pande zote mbili, CCM na CHADEMA walioandika
barua ya kuomba kuahirishwa kwa kesi hiyo baada ya kifo cha mzazi wao ambaye
maziko yake yanatarajiwa kufanyika Septemba 22, 2012.
Jaji Mkuu ametoa amri fupi ya Mahakama kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alikuwa anajibu maombi wa pili aunganishwe kama mtu muhimu katika kesi hiyo.
Kesi hiyo ambayo imesikilizwa kwa takribani saa mbili chini ya Jaji Mkuu na Majaji wengine wawili wa Rufani, ni ya kukata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (CHADEMA).
Mara baada ya kesi hiyo kuhairishwa, umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi katika ofisi za CHADEMA ambapo Lema aliongea na wananchi waliokuwa wakimsindikiza na kuwasihi kuwaombea Majaji wa kesi hiyo ili waweze kutoa hukumu ya haki, “mimi sio kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni zetu za udiwani rasmi,” alisema Lema.
Katika kesi hiyo, Lema anatetewa na Tundu Lissu, wakati kaka yake, Alute Mughwai, anawatetea walalamikaji.
Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dkt. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.
Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.
Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

Kamanda lema akiwa nje ya mahakama |
Kamanda Lema wakati anaingia Mahakamani leo |
Wananchi wa Arusha mjini wakimsikiliza Kamanda Lema kabla ya kwenda mahakamani leo. |
No comments:
Post a Comment