MBUNGE wa Arumeru Mashariki,
mkoani Arusha, kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw.
Joshua Nassari, ameshikilia msimamo wa kupiga marufuku Mwenge wa Uhuru kufika
jimboni kwake na kuwataka wananchi kuupuuza akidai hauna tija kwa maendeleo
yao.
Aliwataka wananchi jimboni
humo wakae mkao wa kula kwani jitihada za kuyatwaa mashamba makubwa
yanayomilikiwa na wageni, zinaendelea hivyo wawe wavumilivu.
Bw. Nassari aliyasema hayo
mwishoni mwa wiki katika mkutano wa hadhara wa Operesheni Sangara uliofanyika
kwenye Kata ya Usa River, wilayani humo.
Aliwaataka wananchi kuupuuza
mwenge huo, kutoshiriki kuchangia mchango wowote na kusisitiza kama mtu yeyote
atabughudhiwa kutokana na ujio wa mwenge amualifu.
“Sioni sababu ya Mwenge wa
Uhuru kukimbizwa maeneo mbalimbali nchini kwani badala ya kuhamasisha maendeleo,
umegeuka sehemu ya ufujaji wa fedha za wananchi.
“Hali hii inachangia umaskini
wa Taifa na kuhamasiha maovu katika maeneo yote ambayo mwengu huu unalala,
nasema hivi, Mwenge wa Uhuru marufuku kufika jimboni kwangu.
“Mtu yeyote ambaye ataombwa
mchango kwa ajili ya mwenge muiteni mwizi na mimi nitakuwa wa kwanza kuuzima
baada ya kufika jimboni kwangu,” alisema Bw. Nassari.
Aliwataka wananchi hao
kuendelea kushiriki shughuli za maendeleo bila kujali itikadi zao kisiasa na
kuihadharisha Halmashauri ya Meru kuzingatia maadili ya utendaji kazi na kuacha
kuwabughudhi wananchi kwa kuwachukulia bidhaa zao hasa wanapokusanya ushuru
sokoni kupitia wakala wao.
Akizungumzia suala la uvamizi
wa mashamba, Bw. Nassari
aliwataka wananchi kuwa
wapole kwani anaandaa mkakati wa kuhakikisha ndani ya miaka mitatu, wamiliki wa
mashamba hayo wanakimbia wenyewe ili wananchi waweze kujitwalia ardhi
yao.
Katika hatua nyingine, Bw.
Nassari alisema fedha zilizotengwa na halmashauri kwa maendeleo Kata ya Usa
River, kuanzia Julai mosi mwaka huu hadi June mwaka 2013, ni sh. milioni 54.3
ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na huduma ya maji safi.
Alisema ukarabati wa barabara
kutoka Usa River hadi Magadilishu umetengewa sh. milioni nane na barabara za mji
mdogo katika kata hiyo zenye urefu wa kilometa tano, zitagharimu sh. milioni
75.
Katika mkutano huo, wafuasi
15 kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Tanzania Labour Party (TLP) walitangaza
kuvihama vyao vyao na kujiunga CHADEMA.
Majira
No comments:
Post a Comment