CHADEMA kupitia makada wake
maarufu, James ole Millya na Jafary Michael walitoa kauli hiyo kwa nyakati
tofauti wakati wa mikutano ya hadhara iliyoanza hivi karibuni katika maeneo
mbalimbali ya mji wa Moshi kutoa ufafanuzi kwa wananchi wa hatua ya mkuu huyo wa
mkoa kuzuia safari hiyo huku wakiita ni ya kisiasa zaidi.
Mapema mwezi huu, Gama
aliwaambia waandishi wa habari mbele ya kamati ya ulinzi ya mkoa kuwa amesitisha
safari hiyo ambayo ingegharimu sh milioni 123.2.
Akizungumza katika mkutano
wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Penford vilivyoko katikati ya mji wa
Moshi, Meya wa manispaa hiyo, Jafary Ally, alisema fisadi yeyote anapothibitika
anachukuliwa hatua za kisheria.
“Ndugu zangu wananchi wa
Moshi, kama kweli Gama anaona kile madiwani wa CHADEMA walichotaka kukifanya ni
ufisadi….. leo hii hakuna hata mmoja wetu ambaye angekuwa katika eneo hili la
mkutano, wote tungekuwa gerezani.
Alisema mkuu huyo wa mkoa
sasa ameacha majukumu yake ya kiserikali na kuanza kutumika kisiasa na Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwa lengo la kuwagombanisha madiwani hao ambao wengi wao
wanatoka CHADEMA.
Meya Michael alisema fedha
zilizotengwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo madiwani zitatumika kama
zilivyopangwa na kama mkuu huyo wa mkoa akiendelea kutumika kisiasa na kuacha
shughuli za utendaji wa kuwatumikia wananchi, watatangaza mgogoro naye wa
kutoshirikiana kwenye shughuli zozote.
Tanzania
Daima
No comments:
Post a Comment