CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) kinatarajia kuzindua matawi katika kila kata nchini, ili
kujihakikishia ushindi wa asilimia kubwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa
utakaofanyika mwaka 2014 nchi nzima.
Kauli hiyo ilitolewa
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, katika
ziara ya ufunguzi wa matawi na msingi 10 ya chama hicho kata ya
Kimara.
Akizindua tawi la Kilungule
‘B’, Mnyika aliwaambia viongozi wa matawi hayo kuziona ofisi hizo kama mbadala
wa ofisi za Serikali za Mtaa zinazoongozwa na CCM kwa kuwasaidia
wananchi.
Aliwataka viongozi hao
kutumia changamoto na matatizo wanayopelekewa na wananchi kuwabana wenyeviti wa
serikali za mitaa, ili kuhakikisha hawarudi mwaka 2014.
“Ndugu zangu wa Kilungule
‘B’ pamoja na changamoto za kisiasa mlizokuwa nazo mmefanikiwa kujenga ofisi za
matawi na misingi … zitumieni vizuri, ili tuweze kupata ushindi mkubwa katika
chaguzi zinazokuja,” alisema.
Mnyika pia amewakabidhi
viongozi wa matawi hayo taarifa za mipango na matumizi ya maendeleo ya jimbo lao
ili kuhakikisha wanafuatilia kwa karibu mambo yanayotekelezwa na yasiyotekelezwa
na serikali.
pamoja na mambo mengine,
Mnyika alitumia fursa hiyo kutoa mwongozo wa kudai Katiba mpya, ili kuhakikisha
mwaka 2015 wanapata Katiba itakayowaondolea dhuluma nyakati za uchaguzi
mkuu.
Tanzania
Daima
No comments:
Post a Comment